Na. Cosmas Mathias Njingo. GAIRO
Aprili 27.2024
Kwa niaba ya wawekezaji wenzangu wa hapa Gairo, tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama yetu kipenzi Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji na kutambua umuhimu wetu katika kuongeza Uchumi wetu binafsi na jamii kwa ujumla.
Shukrani hizo zimetolewa na Bw. Edes Mziwanda Mkazi wa Gairo na Mmiliki wa Nyumba ya kulala wageni ya J5, mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Ndg. Godfrey Mnzava wakati wa mbio za mwenge wa Uhuru 2024 zilipofika kukagua na kuona shughuli za maendeleo zinazotekelewa na sekta binafsi.
Akitoa taarifa za utekelezaji wa Mradi huo, Bw. Mziwanda alimwambia Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kuwa, ujenzi wa Mdadi wa Nyumba ya kulala Wageni ya J5 ulianza kutekelezwa mwaka 2017 baada ya kuonekena kuwepo na mahitaji makubwa ya Nyumba za kulala wageni kutokana na kasi ya ukuaji wa Mji wa Gairom.
“Ndg Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaja 2024, utekelezaji wa mrdai huu ulianza mwaka 2017, hii ni baada ya kuona kuwa kuna mahitaji makubwa ya huduma za malazi kutokana na mwingiliano wa shughuli za kijamii ambazo zimesababisha kasi katika ukuaji wa mji wa gairo”. Alisema Muwekezaji huyo.
Mradi wa ujenzi wa Nyumba ya kulala Wageni ya J5 upo katika kitongoji cha Ukwamani kata ya Ukwamani Tarafa ya Gairo, ambapo jengo la nyumba 11 vyq kulalam huku ukitarajiwa kuwa na tija kubwa kwa Wakazi wa Gairo kutokana na kuzalisha ajira mbalimbali sambamba na kukuza kipato cha mmiliki na Wananchi wengine.
“Ni matarajio yangu kuwa Mradi huu ukikamilika na kuanza kutoa huduma utakuwa na faida kubwa ndani ya Wilaya yetu, ikiwepo kutoa huduma bora za malazi kwa wageni,kuoongeza ajira kwa wananchi hasa vijana na Wanawake, kuongeza mapato ya Serikali kupitia ushuru na kodi mbalimbali pamoja na kukuza uchumi wa Wilaya yetu kutokana na mzunguko mkubwa wa fedha kuendelea kuwepo ndani ya Wilaya ya Gairo” alisema Muwekezaji huyo
Kwa mujibu wa Mziwanda, ujenzi wa Nyumba hiyo ya kulala wageni umegharimu kiasi cha Shilingi 180,000,000.00 hadi kukamilika kwake, kati ya hizo fedha binafsi za mwekezaji ni Shilingi 140,000,000.00 na Shilingi 40,000,000.00 ni za mkopo kutoka Benki
Mbio za mnwenge wa uhuru 2024 zinaongozwa na kauli mbiu inayoisema “Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu”
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa