Na, Cosmas Mathias Njingo
Gairo, Morogoro
Sepetemba 18.2022
“Mtoto wa kiume halazimishwi kuacha shule, lakini mtoto wa kike analazimishwa kuacha shule na kubebeshwa majukumu ya kifamilia yasiyo lingana na umri wake tofauti na mtoto wa kiume”
Afisa Ufuatiliaji na Tathimini, Kutoka Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Morogoro Bw. Ambonisye Haule (Picha Na. Cosmas Mathias Njingo-GAIRO)
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Ufuatiliaji na Tathimini, Kutoka Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Morogoro Bw. Ambonisye Haule, wakati wa Kikao cha Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Mwaka la Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs) Wilaya ya Gairo, uliofanyika Septemba 14, 2022, katika ukumbi wa mikutano wa Halmshauri.
Bw. Haule alibainisha kuwa mila kandamizi zimekuwa zikibagua utoaji wa haki kwa watoto wa kike huku watoto wa kiume wakipewa upendeleo kwenye mgawanyo wa majukumu na ushiriki maamuzi ya umiliki wa rasilimali za familia.
Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Nguzo Imara, Bw. Stiphene Majumba, akichangia mada katika kikao hicho (Picha na Cosmas Mathias Njingo-GAIRO)
Naye Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Nguzo Imara, Bw. Stiphene Majumba alisema Watoto wa Kike kuacha shule na kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi kabla ya wakati, ndoa na mimba za utotoni, husababishwa na Wazazi wenyewe.
Bw. Majumba akaongeza kuwa bado baadhi ya Makabila Wilayani Gairo yanaendelea kufuata mila kandamizi hali ambayo inachochea vitendo vya ukatili wa kijinsia na kingono kwa watoto wa kike, na kuongeza kuwa mila hizo zinawanyima haki watoto wa kike kupata elimu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa