Cosmas M. Njingo
GAIRO
Januari 9.2023
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame, amewataka Wazazi na Walezi kushirikiana na Walimu katika kuhakikisha wanafuatilia mienendo ya watoto wao wawapo shuleni ili kubaini maendeleo yao, kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kuinua kiwango cha elimu na kuongeza ufaulu.
Ametoa rai hiyo Januari 20.2023 wakati wa ziara yake kutembelea shule kwenye kata mbalimbali katika maadhimisho ya wiki ya Elimu Gairo, iliyoambatana na shughuli mbalimbali ikiwepo utoaji wa elimu kwa jamii na wadau wa elimu, ya umuhimu wa wazazi na walezi kushiriki kusimamia sekta ya elimu, ili kuhakikisha watoto wanapata elimu bora itakayosaidia kuondoa sifuri na kuinuwa kiwango cha ufaulu.
“Jukumu la kuhakikisha watoto wetu wanapata elimu na elimu bora siyo la walimu peke yake, Wazazi na Walezi na jamii nzima inahusika. ili kutimiza malengo hayo ni lazima kuwepo na ushirikiano baina ya wadau wote wa Elimu”. Alisema Mhe. Makame.
Mkuu huyo wa Wilaya akaongeza kuwa dira ya Wilaya yake, ni kuhakikisha ufaulu unaongezeka kwa ngazi zote kuanzia darasa la awali gadi kidato cha Nne, na kwamba jamii kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa kuhakikisha anatimiza wajibu wake.
“Tunataka kuona ufaulu unaongezeka kwa ngazi zote za madarasa ambayo mtoto anapaswa kufikia. Shabaha yeti nikuhakikisha Mtoto anafaulu vizuri darasa la awali kuelekea elimu ya Msingi, vivyohivyo tuondoe sifuri kwa wanafunzi wa Darasa la pili kuingia la tatu, darasa la nne kuingia la tano, darasa la saba kuingia kitado cha kwanza, kadhalika kwa elimu ya sekondari lazima ufaulu uongezeke”. Alisisitiza Mkuu huyo wa Wilaya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa