Na Cosmas Mathias Njingo GAIRO
Julai 2.2024
Miezi michache baada ya Baraza la Wahe. Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Gairo kuridhia na kupitisha Sheria ndogo ya halmashuri ya kudhibiti Sumukuvu nabaadae kuwasilishwa Ofisi ya Rais Tamisemi kwa ajili ya kupata kibali cha Waziri. Waziri mwenye dhamana hiyo ameridhiana kusaini sheria hiyo ianze kutekelezwa.
Julai 2. 2024 kilifanyika kikao kazi kati ya ujumbe kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi kwa ushirikiano wa Wizara ya Kilimo na Umwagiliaji na kuwakutanisha Maafisa Watendaji wa Kata kwa lengo la kuwajengea uwezo Maafisa hao kutambua matakwa ya sheria na adhabu zake dhidi ya watakaoenda kinyuma na sheria hiyo.
Afisa Kilimo Mkuu kutoka OR Tamisemi, Dkt. Rehema Mdendemi, alisema wakati wa kikao jhicho kuwa Waziri mwenye dhamana alipokea mapendekezo yaliyotolewa na Baraza la Waheshimiwa, baada ya kuipitia kwa kina ameridhia kuisaini ili ianze kutumika kwa lengo la kudhibiti vitendo vinavyosababisha uwwepo wa Sumukuvu kwenye Mazao
“Waziri ameridhia na kusaini sheria hii, nasi tumekuja tupitishane hatua kwa hatua kujua nini kilichomo, ili ikawe rahisi kwetu sote kuitekeleza. Uzuri ni kwamba watunzi wa Sheria hii ni ninyi wenyewe kwani mchakato wa kukusanya maoni ulianzia ngazi za vijiji na Kata kabla ya kufika Halmashauri”. Alisema Dkt. Mdendemi.
Naye Afisa Kilimo Mkuu, Wizara ya Kilimo na Umwagiliaji Bi. Esther Mwasango, aliwaambia Watendaji hao kuwa Sumukuvu ni tatizo kubwa nchini, na nijanga la Kitaifa na kuongeza kuwa endapo Wananchi hawatazingatia kanuni bora za uhifadhi wa mazao madhara yake ni makubwa kwa afya za Binadamu, hivyo sheria hiyo imekuja wakati muafaka ili kuchukua hatua za kukomesha madhara yanayotokana na Sumukuvu kwenye vyakula.
“Halmashuri iliamua kutengeneza Sheria ndogo, ambayo itatumika kudhibiti vitendo vinavyosababisha sumukuvu kwenye mazao na kuleta madhara kwa afya ya binadamu, na hapa wapo Watendaji wa Kata zote, lengo ni kujua dhabu zipi zinapaswa kutekelezwa endapo mwamanchi yoyote atakiuka matakwa yaliyotajwa na Sheria hii”. Alisema Mtaalam huyo.
Mchakato wa uundwaji wa Sheria ndogo hiyo ya Halmashuri ya kudhibiti sumukuvu kwenye mazao ulianzia ngazi za vijiji kwa Wananchi kushiriki kutoa mapendekezo ya rasimu ya sheria hiyo, kujadiliwa kwenye vikao vya maendeleo vya kata na baadaye kuwasilishwa kwenye Baraza la Madiwani kisha kupelekwa kwa Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi ambaye ameridhia mapendekezo ya Sheria hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa