Wachimbaj wa wadogo wa madini waligundua upatikanaji wa madini hayo mwanzoni mwa mwezi Juni, 2019 jambo ambalo lilisababisha wachimbaji wengi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi kufurika katika eneo hilo. Baada ya kubainika kuwa zipo shughuli za uchimbaji wa madini aina ya dhahabu katika kijiji cha Kilama Kata ya Iyogwe Wilayani Gairo, Kamati ya ulinzi na Usalama ya Wilaya, Afisa madini Mkazi wa Mkoa wa Morogoro pamoja na Mkurugenzi Mtendaji na Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Gairo mnamo tarehe 8 Juni, 2019 walifanya ziara katika eneo hilo ili kuzungumza na wachimbaji hao pamoja na kuweka utaratibu mzuri wa namna uchimbaji unavyoweza kufanyika kwa manufaa ya pande zote.
Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Bi. Sirel Mchembe ambaye ndiye Mkuu wa Wilaya aliongoza kikao hicho ambapo waliazimia mambo yafuatayo:-
Aidha, wachimbaji walielezwa faida ya uchimbaji kama watatumia utaratibu mzuri, wao watanufaika na uchimbaji huo na serikali nayo kutapata mapato
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa