Na. Cosmas Mathias Njingo, 88 MOROGORO
Agosti 7. 2023.Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jaffo (Mb) amewataka Wananchi hususani wakulima, kuwa msitari wa mbele katika kuendeleza juhudi za Serikali za utunzaji na uhifadhi wa mazingira ili kuepukana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yanaathiri sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, ufugaji na uvuvi.
Waziri Jaffo ametoa wito huo Agosti 8 mwaka huu wakati akizungumza na Waandaishi wa habari baada ya ziara yake ya siku moja ya kutembelea mabanda na vipando vya mazao mbalimbali katika maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki katika viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
“Hii swala la mabadiliko ya tabia Nchi tumejionea wenyewe namna ambavyo linaathiri sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi; nah ii inatokana na wingi wa shughuli za kibinadamu zisio zingatia uhifadhi na utunzaji wa Mazingira. Hivyo ninatoa rai yangu kwa kwa Wananchi wote na hasa hasa Wakulima kuhakikisha wanakuwa atunzaji namba moja wa mazingira.
Kawa upande mwingine Waziri Jaffo amepongeza Uongozi wa Kanda ya Mashariki kwa namna ambavyo umejipanga katika kuwezesha na kufanikisha maonesho ya Nanenane kwa kanda hiyo; na kwamba maonesho hayo yanaenda kuleta mabadiliko makubwa kwa Wakulima na Wadau wa Sekta hizo kwani yametafasiri kwa vitendo dhana ya Mhe. Dakta Samia Suluhu Hassan, ya Wakulima kupata tija katika shughuli za Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
“Binafsi nimefarijika sana na maandalizi mazuri ya maonesho ya Wakulima ya mwaka huu katika kanda hii ya Mashariki, nahii inatoa fursa kwa Kanda ya Mashariki kuendelea kuwa kinara wa maonesho ya Nanenane Tanzania kutokana na namana ambavyo mmejipanga kwa maandalizi na mpangilio wa mabanda ya maonesho, bidhaa zilizopo na hata ushiriki wa Wadau mbalimbali unaridhisha sana”. Alisema Waziri Jaffo.
Kwa upande wake Mhe. Adam Kighoma Malima, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na mwenyeji wa Maonesho hayo, alisema Kanda ya Mashariki inajukumu la kulinda mazingira kutokana na umuhimu wa mito inayopeleka maji katika bwawa la kufua umeme la Mwl. Nyerere linalotarajia kuzalisha umeme zaidi ya Megawati 2000.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa