Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, imekabidhiwa rasm ghara la kisasa lenye miundombinu muhimu ya kudhibiti sumukuvu baada ya ujenzi wake kukamilika
Ujenzi huo uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni moja, umetekelezwa na Wiraza ya Kilimo, na Umwagiliaji, kupitia mradi wa TANPAC, na kujengwa katika kijiji cha Kimashale kata Chakwale unatarajiwa kuleta tija kubwa kwa wakulima wa zao la Mahindi na Karanga ambayo yanatajwa kuwa mazao pekee yanayoathiriwa na kuvu kwa kiwango kikubwa.
Ujenzi huo umehusisha majengo manne likiwepo Jengo la Ghala lenye Uwezo wa kubeba tani za mazao 1,500, Ofisi, Maabara na Kibanda cha Mlinzi.
Miundimbinu mingine ni sehemu ya kuanikia mazao, Kihenge cha kuhifadhia taka, tangi la maji la ujazo wa lita 20,000 na vifaa vya tahadhari kama ving'ora.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa