(wajumbe wa Kamati ya Lishe Wilaya, katika kikao cha Kamati Julai 11.2022 ukumbi wa mikutano wa Halmashauri)
Na. Cosmas Mathias Njingo. GAIRO DC
Ushauri umetolewa kuundwa kwa sheria ndogo za Halmashauri kwa ajili ya kutekeleza agizo la serikali la kuwataka wazazi kuchangia chakula mashuleni ili kuwabana Wazazi na Walezi wanaokaidi agizo hilo hali inayochangia utoro kwa wanafunzi na kusababisha ufaulu hafifu.
Ushauri huo umetolewa na wajumbe wa Kamati ya Lishe Wilaya wakati wa kikao cha Kamati hiyo cha kujadili taarifa za robo ya nne kwa kipindi cha Aprili-Juni 2022 pamoja na kupitia viashiria vya mkataba wa Lishe kwa kipindi cha Julai 2021-Juni 2022, kilichofanyika Julai 12.2022 karika ukumbi wa Halmashauri.
(Kaimu Afisa Mipango (W). Ndugu Paulo Sangiwa (mwenye miwani) akifuatiwa na Afisa Elimu Maalum Mwalimu Peter Japhet na Kaimu Mkuu wa Idara ya
Kilimo Ndugu Stephen Majumba)
Akichangia taarifa ya hali ya utoaji chakula shule za Msingi na Sekondari iliyowasilishwa na Mwalimu Peter Japhet kwa niaba ya Wakuu wa Idara za Elimu Msingi na Sekondari, Afisa Habari Mawasiliano na Uhusiani Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Bwana Cosmas Njingo alisema ipo haja ya Idara hizo mbili kuona namna ya kuweka mkakati wa kutunga sharia ndogo kwa ajili ya kuwabana Wazazi na Walezi wanao kaidi agizo la Serikali la kuwataka kuchangia chakula ili kuwawezesha wanafunzi kupata chakula cha mchana mashuleni.
“Ushauri wangu kwa idara hizi mbili, zianzishe mchakato kupitia Ofisi ya Afisa Sheria wa Halmashauriwa kuandaa rasimu ya Sheria ndogo za kuwabana Wazazi na Walezi wanaokaidi kwa makusudi agizo halali la Serikali linalowataka wazazi wote kuchangia vyakula mashuleni kwa ajili ya watoto wetu”.
(Mratibu wa Lishe (W) Bi. Loveness Achimpota na Afisa Lishe wa Mradi wa Lishe Endelevu unaotekelezwa na Taasisi ya CEMDO Ndugu. John Kiussa)
Msemaji huyo kutoka Kitengo cha Mawasiiano Serikali cha Halmashauri, akaongeza kuwa kuwepo kwa sheria hiyo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa migogoro ambayo inajitokeza hivi sasa kati ya Watendaji wa Kata, Walimu Wakuu pamoja na Wakuu wa Shule na Wazazi kutokana na kukosa nguvu za kisheria katika kuwachukulia hatua Walenzi na Wazazi ambao wamekuwa kikwazo kuhusu utekelezaji wa kuchangia chakula mashuleni.
“Ndugu wajumbe migogoro mingi imeibuka baina ya Wazazi na Watendaji wa Kata, Wakuu wa Shule na Walimu Wakuu, kutokana na baadhi yao kukaidi kwa makusudi kuwachangia vyakula watoto wao, sasa kimsingi Watumishi hawa wanapata shida sana kutekeleza swala hili, maana hakuna sheria ya kuwalinda Watendaji na walimu, lakini pia hakuna sheria inayowapa meno kuchukua hatua kali dhidi ya Wazazi wanao kaidi amaelekezo ya Serikali”. Alieleza Bwana Njingo.
(wajumbe wa Kamati ya Lishe Wilaya, katika kikao cha Kamati Julai 11.2022 ukumbi wa mikutano wa Halmashauri)
Naye Mwakilishi wa Umoja wa Madhehebu ya Kikristo Tanzania (CCT), Peter Kihiyo alisema upo ulazima wa mchakato huo wa utayarushaji wa sheria ndogo kuhusu maswala ya lishe mashuleni na kwamba ufanyike haraka ili kunusuru hali ya ufaulu kwa wanfunzi.
“Mwenyekiti nakubaliana kabisa na mjumbe aliyetoa ushauri huu, ni muhimu utaratibu wa kuandaa Rasimu ya Sheria hii ukamilike haraka ili ipitishwe kwenye vikao vyote muhimu vya kisheria na ianze kutumika mara moja. Hii itasaidia kunusuru hali ya utoro mashuleni kwa wanafunzi kukosa chakula cha mchana”, alisisitiza.
Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Lishe katika robo ya Nne ya kipindi cha Aprili-Juni 2022 Afisa Lishe Wilaya ya Gairo Bi. Loveness Achimpota alisema kuwa Lishe na Utapiamlo ni maswala mtambuka katika jamii na husababisha matatizo mengi.
(Mratibu wa Lishe (W) Bi. Loveness Achimpota) aliyesimama akiwasilisha mada, waliokaa kutoka kushoto ni Kaimu Katibu wa Mikutano Ndugu Abuu Liwangila na Afisa Habari Ndugu Cosmas Njingo)
“Lishe ina athari kubwa kwa makundi maalum kama watoto wa chni ya umri wa miaka mitano, wajawazito na akina mama wanaio nyonyesha. Hivyo ni wajibu wakila mjumbe kuhakikisha anawajibika kutoa elimu kuhusu maswala ya umuhimu wa Lishe kwa jamii ili kuepusha matatizo kama utapiamlo na vifo kwa watoto”, aliwasilisha Afisa huyo.
(Mratibu wa Lishe (W) Bi. Loveness Achimpota) aliyesimama akiwasilisha mada,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa