Kazi ya ujenzi wa jengo la vyumba 2 vya madarasa na ofisi katikati shule ya msingi Chakwale, Kata ya Chakwale Wilaya ya Gairo. Jengo hili limegharimu kiasi cha Tsh.40m kutoka serikali kuu kwa ajili ya kupandisha boma na kumalizia miundombinu yote ikiwepo uwekaji wa fremu za milango na padirisha pamoja na top za milango, grili za madirisha, kuweka fremu za alminium kwenye madirisha na vioo vyake, kupaua, kufunga gypsum, kupiga plasta ndani na nje,kuweka miundombinu ya nishati ya umeme, kuweka sakafu ya vikae (tiles). Pamoja na kiasi hicho cha fedha kutoka Serikali Kuu, Wanachi wa Chakwale walichangua nguvu kazi ikiwepo uchimbaji wa msingi, mchanga, kokoto na kupamnga mawe kwenye msingi kwa ajili ya jamvi la chini. Kukamilika kwa mradi huu kutapunguza adha ya wanafunzi kurundikana wengi kwenye darasa moja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa