Wilaya ya Gairo ilianzishwa kwa Tangazo la Serikali Na 75 la tarehe 02/03/2012 kufuatia kugawanywa kwa Wilaya ya Kilosa, na baadaye utekelezaji wa shughuli za Halmashauri ulianza rasmi Julai 2013. Gairo inapatikana kaskazini Magharibi mwa Mkoa wa Morogoro na inapitiwa na barabara kuu ya Morogoro-Dodoma.
Eneo la Wilaya ni Kilometa za mraba 1,851.34. inapakana na Wilaya ya Kongwa na Mpwapwa kwa upande wa Magharib, kilosa ipo Kusini na kwa upwande wa Mashariki zipo Kilosa na Mvomero. Aidha upande wa Kaskazini inapakana na sehemu ya Wilaya za Kongwa na Kiteto.
Gairo inakadiriwa kuwa na wakazi wapatao 193,011 (Me 93,206 na Ke 99,805, hii ni kwamujibu wa Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012. Wastani wa watu kwa kaya ni 5.2 sawa naongezeko la asilimia 2.6 kwa mwaka.
Wilaya inaundwa na Tarafa mbili , Kata 18, vijiji 50 na vitongoji 304 (23 kati ya hivyo viko chini ya Mamlaka ya Mji Mdogo wa Gairo) . Lipo jimbo moja la uchaguzi la Gairo. Jumla ya madiwani 24 wakiwemo 18 wa kuchaaguliwa na 6 ni viti maalumu.
Kauli mbiu yetu ni "Ifanye Gairo kuwa Halmashauri kubwa kimapato"
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa