(Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza na Maafisa Habari wa Taasisi, Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya kwenye kikao kazi cha siku moja kilichofanyika Ofisi za Mkuu wa Mkoa Dodoma Julai 1.2022)
Na. Cosmas Mathias Njingo, GAIRO DC
Wakuu wa Mamlaka za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Nchini wametakiwa kuhakikisha wanatangaza fura muhimu za maendeleo zinazopatikana katika maeneo yao sambamba na kutoa taarifa muhimu kwa jamii kuhusu shughuli zinazotekelezwa na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan ili kuiwezesha Umma kufahamu namna ambavyo Serikali yao inatekeleza shughuli za kuwaletea maendeleo kwa kuwatumia kikamilifu Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini waliopo kwenye Mamlaka zilizopo chini ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI.
((Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza na Maafisa Habari wa Taasisi, Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya kwenye kikao kazi cha siku moja kilichofanyika Ofisi za Mkuu wa Mkoa Dodoma Julai 1.2022)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa (MB) ametoa agizo hilo Julai 2.2022 wakati akifungua kikao cha siku moja cha Maafisa Habari, Mahusiano na Itifaki Serikalini waliopo kwenye Taasisi na Mamlaka zilizopo chini ya Wizara yake, kilicho fanyika katika ukumbi wa mikutano ofisi za Mkuu wa Mkao wa Dodoma.
"Nina waagiza Viongozi wote wa Taasisi zilizopo chini ya Wiraza yangu, Makatibu Tawala wa Sekretarieti za Mikoa na Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Halmashauri zota za Wilaya nchini wanawatumia vizuri na kuhakikisha wanawasimamia vyema Maafisa Habari na Uhusiano waliopo kwenye Mamlaka zao kutekeleza majuku yao kikamilifu ya kuhabarisha Umma ili kuiwezesha jamii ya maeneo husika kupata taarifa muhimu za kuwawezesha kufahamu maswala mbalimbali ya kimaendeleo yanavyotekelezwa na Serikali yao kwa maslahi mapana ya kuletea maendeleo". Alisema Mhe. Bashungwa.
Mhe. Bashugwa amesema kuwa ni wajibu wa Viongozi hao kuhakikisha wanaitumia Timu ya Maafisa Habari waliopo chini yao kutangaza miradi ya Maendeleo inayotekelezwa nchi nzima ili kuwapasha habari wananchi kuhusu kazi kubwa inayofanywa na Serikali, lengo ikiwa ni kuwajengea uelewa wananchi kufahamu miradi ya maendeleo inayo tekelezwa na Serikali yao.
(Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais TAMISEMI Bi. Nte akitoa maelekezo kwa Maafisa Habari Serikalini)
“Serikali inatoa fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha huduma mbalimbali kwa Wananchi wake, pamoja na kutengeneza miundombinu ya kuibua fursa za maendeleo na kukuza uchumi, hivyo ieleweke kwamba suala la kuhabarisha Umma kuhusu utendaji kazi wa Serikali yao ni muhimu, na kwamba si jambo la hiari bali ni lazima kila kiongozi kwa nafasi yake ana wajibu kuhabarisha umma juhudi za Serikali katika kuwatumikia Wananchi," alisitiza Waziri Bashungwa.
Amefanunua kuwa katika mwaka wa fedha 2022/2023 serikali inapanga kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ambayo italeta mageuzi makubwa ya Kiuchumi kuanzia ngazi ya mwananchi mmoja mmoja hadi Taifa kwa ujumla hivyo ni vyema upatikanaji na utoaji wa taarifa ukaanzia ngazi zote za jamii kutoka Kijiji , Mtaa, Wilaya, Mikoa na Taifa kwa ujumla ili kila mtanzania aweze kuwajibika katika eneo lake.
Aidha Waziri Bashungwa amewataka viongozi hao kuhakikisha wanafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na Maafisa Habari wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na kuwasimamia ili waweze kutimiza wajibu wao wa kuhabarisha Umma kwa wakati kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo ya Utumishi wa umma, na kuongeza kuwa kila mmoaja akitimiza vizuri majukumu yake kwa weledi katika kutoa taarifa taarifa sahihi kwa umma kutaondoa malalamiko ya Wanachi dhidi ya serikali na upotoshaji kuhusu matumizi ya fedha za Umma kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.
(Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Charles Msonde)
Naye, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Charles Msonde amewahimiza Maafisa Habari hao wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanawafikia Wananchi kwa kuwapa taarifa sahihi na muhimu kupitia tovuti na mitandao ya kijamii ya Taasisi zao ili kuongeza uelewa kwa jamii kwa kuonyesha kwa vitendo namna Serikali ya awamu ya Sita inavyo wahudumia Wananchi wake.
Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO, Gerson Msigwa amewataka Maafisa habari wote nchini kutumia radio na television za kijamiii katika maeneo yao kutangaza mafanikio na agenda ya Kitaifa pamoja na kutokukaa kimya dhidi ya taarifa za upotoshaji zinazolenga kuleta mtafaruku na kuzua taharuki kwa Wanachi ambazo zinaweza kusababisha kuchochea chuki kati ya Wananchi na Serikali yao.
(Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Ndugu Gerson Msigwa akizungumza na Maafisa Habari wakati wa Kikaoa kazi cha siku moja jijini Dodoma Julai 1.2022)
"Kwa haraharaka Maafisa wa Habari serikalini ni zaidi ya mia tatu, kwa wingi huu ninashangaa kuona mpo kimya tu hamsemi kitu pale baadhi ya watu wachache wanapotoa taarifa za upotoshaji zenye kuzua taharuki kwa Wananchi, taarifa mbaya kuhusu Serikali zinapostiwa kwenye mitandao ya kijamii lakini sioni yeyote kati yenu akiposti majibu na kuweka ukweli kuhusu tuhuma chafu za kuichafua serikali". alishangaa
Kikao hucho cha siku mbili kilihudhuriwa wa Maafisa Habari na Uhusiano kutoka Mamlaka ya Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Halmashauri za Wilaya pamoja taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kiliambatana na mada mbalimbali zilizotolewa kwa lengo la kuwajengea uwezo Watendaji hao wa Sekta ya Mawasiliano Serikalini ambapo siku ya pili walipata fursa ya kutembelea na kujionea shughuli za ujenzi wa Ofisi za Umma katika Mji wa Kiserikali Mtumba na Ujenzi wa mradi wa Soko kubwa la kisasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa