Na. Cosmas Mathias Njingo. GAIRO,
Juni 4.2024
Halmashauri ya Wilaya ya Gairo imeendelea kuimarisha usimamizi na utekelezajai wa shughuli za ukusanyaji wa mapato, ambapo inatarajia kufikisha 100% ya lengo la ukusanyaji ifikapo Juni 2024.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri hiyo Bi. Sharifa Nabalang’anya wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Maendeleo kwa Waheshimia Madwani katika katika kikao cha Baraza la kupokea na kujadili taarifa za robo ya tatu kwa kipindi cha Januari-Machi 2023/2024 kabla ya kumribisha Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Rahel Nyangasi kufungua Mkutano huo, uliofanyika Mei 24.2024 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmasha.
“Mhe. Mwenyekiti, tumefanya vizuri kwenye ukusanyaji wa mapato kwa kipindi cha robo iliyopita ya Januari-Machi 2023/2024. Ni matarajio yetu kuwa ifikapo Juni 30 tutafikia 100% ya ya makusanyo ya mapato kwa lengo tulilokuwa tumejiwekea”. Alisema Bi Sharifa.
Akifungua Mkutano huo Mh. Raheli Nyangasi alimopongeza Mkurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Divisheni na Vitengo, Timu ya Kukusanya Mapato na Maafisa Watendaji wa Kata kwa usimamizi mzuri katika kutekeleza jukumu hilo la kukusanya mapato na kuiwezesha Halmashauri kufikia 83% ya lengo.
“Nichukue fursa hii kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji na timu nzima ya Wataalam kwa kazi nzuri mliyoifanya. Kwakweli tumeona na tumeamini kwamba kazi inaendelea vizuri, kwani hadi jana inaonesha tumefikia 83% ya lengo. Ni matarajio yetu kuwa kwa kipindi kilichobakia tutafika 100% na kuvuka kabisa lengo la Makusanyo kwa mwaka 2023/2024”. Alipongeza Mwenyeiti huyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa