Wilya ya Gairo imepokea na kukimbiza Mwenge wa Uhuru 2021 katika jumla ya miradi 7 ambapo kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Luteni Josephine Mwambashi amewapongeza vingozi wote, watumishi na Wananchi kwa ujumla wao kwa kufanya vizuri utekeleza miradi hiyo.
Agasti 9, 2021 mwenge ulipokelewa katika kijiji cha Tabu hoteli kata ya Chigela ukitokea Wilaya ya Mvomero kisha ulifika Sekondari ya Kibedya kukagua Mradi wa Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa.
Pia mwenge huo ulifika Madoto kijiji cha Mogohingwa na kujionea ujenzi wa Zahanati. Miradi mingine iliyotembelewa na mwenge ni pamoja na kuona mtambo wa kuchakata na kuchuja maji chumvi kwa njia ya teknolojia ya kisasa unaosimamiwa na kampuni ya Protecno.
Miradi mingine iliyo onwa na mwenge wa Uhuru ni maendeleo ya ujezi wa nyumba ya kulala wageni Majaliwa iliyopo Ukwamani, Kitalu cha zao bora la Mokonge, uzinduzi wa club ya kupambana na rushwa shule ya Msingi Lolela na Msingisi pamoja na kikundi cha vijana Rubeho Transporters wanao fanya biashara ya boda boda.
Wakimbiza mwenge kitaifa wakiongozwa na Luteni Josephine Mwambashi waamesema wmefurahishwa na ushirikiano walio onyeshwa kwenye miradi yote na kwamba kila kilicho hitajika kilikuwa kipo sawa hivyo wamepokea taarifa za miradi yote na wamekubaliana nayo.
Mwenge huo unatarajiwa kukabidhiwa Manispaa ya Mko wa Morogoro Agosti 10 baada ya kukimbizwa Wilayani Gairo na kufuatiwa wa shamra shamra zingi kwenye uwanja wa mkesha uliipambwa kwa hamasa kubwa ya burudani toka kwa wasanii mbali mbali wa muziki wa dance, kizazi kipya, vijana wa Hamasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), matarumbeta, halaiki pamoja na vijana wa skauti.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa