Imeelezwa kuwa jumla ya kaya 6271 zinatarajiwa kushiriki kwenye uundaji wa vikundi vya kuweka akiba na kuwekeza kwa walengwa wa kaya zinazonufaika na mpango wa TASAF wa kusaidia kaya maskini Wilayani Gairo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Bi Susan Nyanda amebainisha hayo kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo kwa timu ya wawezeshaji wa TASAF ngazi ya Halmashauri kuhusu utaratibu wa uundaji wa vikundi vya kuweka akiba na kuwekeza kwa walengwa wa Mpango, yaliyofanyika Disemba 1.2021 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
“Hapa Gairo tunzao kaya 6271 ambazo zimeingizwa kwenye utaratibu huu wa uundaji wa vikundi vya kuweka akiba na kuwekeza, lengo la Serikali ni kuhakikisha kaya zinajikwamua kiuchumi ili kujiongezea kipato”. Alisema Bi Nyanda.
Kaimu Mkurugenzi huyo akabainisha kuwa katika kipindi cha pili cha utekelezaji wa mpango huu mkazo umewekwa zaidi katika kuziwezesha kaya husika kufanya kazi ili kujiongezea kipato kupitia utekelezaji wa miradi ya kutoa ajira za muda kwa Walengwa, pamoja na kuhamasisha uwekaji wa akiba sambamba na kutekeleza shughuli za kukuza uchumi wa kaya hususani kwa kaya zenye uwezo wa kufanya kazi.
“Tunasisitiza kwamba ni wajibu kuhakikisha tunaweka mkazo mkubwa katika kuziwezesha kaya kufanya kazi, hasa zile kaya zenye uwezo wa kufanya kazi ilikujuiongezea kipatokupitia utekelezaji wa miradi inayotoa ajira za muda mfupi”, alisisitiza Bi Nyanda.
Bi. Nyanda akawaeleza washiriki wa mafunzo hayo kuwa katika kipindi kilichopita Kaya lengwa zilipewa elimu ya stadi za ujasiriamali na mbinu za uundaji vikundi endelevu vya kuweka akiba na kuwekeza, na kwamba zaidi ya Wanachama laki tatu wameunda vikundi vipatavyo 23, 6138 katika Halmashauri 78 Tanzania Bara na Visiwani.
“Kipindi kilichopita tulifanya uhamasishaji na utoaji wa eliku kwa jamii kuhusu uundaji wa vikundi vya kuweka akiba na kuwekeza, hapa Gairo kaya zilizohamasishwa zimeonyesha mwamko mkubwa na ari ya kuunda vikundi ili kutekeleza kwa vitendo elimu tuliyo itoa”, aligusia
Akaongeza kusema “Hapa kwetu Gairo tunatarajia kuunda vikundi vipatavyo 419 kutoka katika kaya 6271 ambapo kila kikundi kitakuwa na wanakikundi kati ya 10 na 15. Kupitia vikundi hivi kuna fursa za kukopa mikopo ya riba nafuu ambayo itasaidia kaya hizo kujikwamua kiuchumi kwa kuweka akiba na kuwekeza kwenye shughuli za uzalishaji mali”, Alibainisha Bi. Nyanda.
Mafunzo hayo ya siku tano yanaendeshwa na timu ya Wataalamu kutoka TASAF makao makuu yatafanywa kwa nadharia na vitendo ambapo Wawezeshaji ngazi ya Halmashauri watatakiwa kwenda kutoa elimu kwa jamii na kuhamasisha uundaji wa vikundi vya kuweka akiba katika vijiji vyao sambamaba na kushiriki katika shughuli za kukuza uchumi wa kaya.
Aidha wawzeshaji hao ngazi ya Halmashauri wametakiwa kukakikisha wanashirikiana na viongozi wa Wananchi ikiwepo Serikili za Halmashauri za vijiji, Wenyeviti wa vitongoji pamoja na Waheshimiwa Madiwani katika kata ambazo zoezi hili litatekelezwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa