Na, Cosmas Mathias Njingo. GAIRO
Juni 3.2024
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mhe. Rahel Nyangasi, amewaasa Wahe. Madiwani wa Halmashauri hiyo, kuongeza kasi ya usimamizi wa ukusanyaji wa mapato kwa kushirikiana na Maafisa Watendaji wa Kata, ili kufikia malengo ya ailimia 100 ifikapo Juni 30. 2024, kwa lengo la kuiwezwesha Halmashauri kupata mapato ya kutosha sambamba na kuhakikisha asilimia 10 zinarejeshwa kwa wakusanyaji wamapato kwa wakati.
Amesema hayo katika hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani wa kupokea na kujadili taarifa za Robo ya Tatu ya Januari- Machi 2023/024 uliofanyika Mei 24.2024 katika ukumbi mkubwa wa Mikutano wa Halmashauri.
“Malengo ambayo tumeyapanga wenyewe tukiyafanikisha inakuwa ni jambo jema sana, lakini pia tuwe tumefanikiwa kwa asilimia 100, ili tuingie mwaka mpya wa fedha 2024/2025 tukiwa na malengo mapya”. Alisema Mhe. Nyangasi
Hata hivyo Mhe.Nyangasi alisisitiza swala la kuwalipa kwa wakati Wakusanyaji wa mapato asilimia zao 10 ya kile wanachokikusanya linapaswa kutiliwa mkazo, kwani kwa kufanya hivyo kunatoa hamasa kwa wakusanya mapato kukusanya kwa bidi na uaminifu mkubwa, na kwamba utaratibu huo utaondoa wizi na njama za utoroshaji wa mazao kati yao na wafanyabiashara wanaosafirisha mazao.
“Kutokurejesha asilimia 10 kwa wakusanyaji ni Wizi, mtambue kuwa hela tunayoitumia kutekeleza shughuli mbalimbali za Halmshauri siyo yetu, ni fedha iliyopaswa kurudishwa kwa wakusanya ushuru. Hivyo tuhakikishe hili nalo tunalisimamia”. Alisisitiza.
Kwa upande mwingine Mhe. Mwenyekiti Amemshukuru Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha nyingi za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani Gairo, ambapo amewakumbusha Wahe. Madiwani hao kushiriki kwenye shughuli za maendeleo katika Kata zao, pamoja na kuhakikisha miradi yote ya maendeleo inatekelezwa kwa ubora unaotakiwa na ikamilike kwa Wakati.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa