Na. COSMAS MATHIAS NJINGO, GAIRO
FEBRUARI 9.2024
Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro, katika mwezi Januari 2024, ilipokea fedha kutoka Serikali Kuu jumla ya Shilingi Bilioni 1, 911, 450,910, kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo kwenye sekta za Elimu, Afya na Utawala; pamoja na kulipa malimbikizo ya Wastaafu.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi. Sharifa Nabalang’anya, mbele ya Wahe. Madiwani; akimkaribisha Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Rahel Nyangasi, kufungua kikao cha Kawaida cha Baraza la Wahe. Madiwani; kilichoketi Februari 9.2024 kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
“Mhe. Mwenyekiti ninapenda kukijulisha kikao hiki cha Baraza la Wahemshimiwa Madiwani kuwa Halmashauri yeti imepokea Fedha kiasi cha Shilingi bilioni Moja nukta tisa moja, laki nne na hamsini elfu mia tisa na kumi kwa ajili ya matumizi ya miradi, malipo ya Wastaafu na malipo mengineyo”. Alisema Bi. Nabalang’anya.
Akitoa taarifa hiyo, Nabalang’anya alisema Shiling 1,256, 837,634 ni za mishahara ya Watumishi, wakati malimbikizo ya Wastaafu 4 ni Shilingi. 4,228,000 huku ruzuku ya matumizi ya kawaida ikiwa imetengewa Shilingi 72,086,000.
Mkurugenzi huyo wa Halmashauri alitaja zaidi matumizi mengine ya fedha hizo; kuwa ni pamoja na Shilingi 84, 219, 358 za Elimu bila ada kwa shule za Msingi na Sekondari, miradi ya ujenzi wa miundombinu shule za Sekondari kwa mwaka 2024 shilingi 319,086,000, Mfuko wa pamoja wa Afya (HSBF-CHMT) shilingi 113,615,750 na shilingi 61,464,168 kwa ajili ya Chanjo za kawaida, GAVI na Kovidi 19 ngazi za chini.
“Mhe. Mwenyekiti ninaomba kutumia nafasi hii kwa moyo wa dhati kumshukuru sana Mama yetu; Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwekeza mapenzi makubwa kwa Wananchi wa Gairo, hasa kutenga fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo”. Alishukuru Bi. Sharifa.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Nyangasi akifungua mkutano huo alisema, Wajumbe wa Baraza hilo la Wahe. Madiwani wamepokea kwa shukrani nyingi salam za upendo kutoka kwa Mhe. Rais Dkt Samia kupitia mgawo wa fedha hizo ambazo alibainisha zinaenda kuleta mbadiliko kwa Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo na kuchochea maendeleo.
Sambamba na shukrani hizo Mhe. Nyangasi aliwaasa Wakuu wa Divisheni na Vitengo na Watumishi wote, kufanya kazi kwa weledi, uadilifu, umakini na uaminifu wa hali ya juu, katika kusimamia utekelezaji wa shughuli za maendeleo ili kuleta matokeo chanya ya matumizi ya fedha hizo zilizotolewa na Serikali.
Baraza hilo mbali na mambo mengine, limepokea na kupitisha taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa kipindi cha Robo ya Pili cha Oktoba-Disemba 203/2024 huku likimsisitiza Mkurugrnzi wa Halmashauri na Timu yake ya Wataalam kuhakikisha maagizo yote yaliyotolewa yakatekelezwe kikamilifu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa