Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Medadi Kalemani ametoa vifaa arobaini vya kuwasha umeme ndani bila kusambaza miundombinu ya waya (wiring).
kifaa hichi kinajulikana kwa jina la UMETA kimewekewa mfumo maalumu wa kuwezesha kuwasha taa zaidi ya nne kwa wakati mmoja pasipo kusambaza nyaya vyumbanina maeneo mengine.
Waziri Kalemani amesema UMETA ni mkombozi kwa wananchi wa kipato cha chini ambao hawana uwezo wa kukunua nyaya, swichi za kuwashia taa, soketi break, meini swichi na miundo mbinu mingine, kwani chenenyewe kimejitosheleza kusambaza umeme (mwanga) ndani ya nyumba.
"UMETA ni kifaa mkombozi kwa wananchi wenye kipato cha chini wasio na uwezo wa kununua vifaa vingi vinavyohitajika kwa ajilikusambaza miundombinu ya umeme ndani ya nyumba", alisisitiza.
Alisema anachotakiwa kufanya mwananchi ni kwenda ofizi za Tanesco kufanya malipo ya Shilingi elfu ishirini na saba tu kisha mafundi wataenda na kifaa hicho kumuunganishia umeme kutoka kwenye nguzo kwa kuzingatia taratibu zote za kumtambua kuwa ni wa kipato cha chini hawezi kugharamia vifaa vya kuweka miundominu ya umeme ndani kwake.
Pamoja na kutoa UMETA arobaini kwa ajili ya kaya 4o za wakazi wenye kipato cha chini pia Waziri kalemani ametoa UMETA nyingine 250 kwa ajili ya vijiji vyote vitakavyo pitiwa na mradi wa umeme wa REA ili wananchi wengi zaidi waweze kunufaika.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa