Cosmas Mathias Njingo; MOROGORO.
Oktoba 1. 2022.
Mkoa wa Morogoro umewatukunu tuzo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, pamoja na Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (MB), ya heshima na ushiriki wao mkubwa kwa kuweka vipaumbele vya kutosha katika kuinua sekta ya kilimo na kuongeza bajeti sambamba na kupunguza bei ya pembejeo za kilimo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Abubakari Mwassa, alitangaza kuwatunuku tuzo hizo Oktoba Mosi 2022, kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa huo, wakati wa kuhitimisha wiki ya Mbio za Kilimo (Kilimo Marathone) lililoambatana na maonesho ya shughuli za kilimo na ufugaji na teknolojia mbalimbali za kilimo.
“Kwa heshima kubwa sana, na kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa wa Morogoro, tunatoa Tuzo ya Heshima ya Mkulima Bora wa Kwanza Tanzania, kwa Rais wetu, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan, pamoja na Mhe Bashe, Waziri wa Kilimo. Hii inaonyesha kuwa tunatambua mchango wake katika kuinua sekta ya kilimo nchini”. Alisema Mhe. Fatma Mwassa.
Mhe. Mwassa alisema kuwa, Rais Samia amedhamiria kwa dhati kuhakikisha kilimo kinainuka Tanzania kwa kupunguza bei ya pemnejeo za kilimo ambapo ametoa ruzuku ya mbolea ili kuwezesha wakulima kupata mbolea hizo kwa bei pungufu kwani serikali nayo italipia nusu ya gharama hizo, ambapo bei ya ambolea imeshuka kutoka Shilingi 120,000 hadi shilingi elfu 60,000 kwa nfuko wa kilo 20.
“Mheshimiwa Rais na Waziri wa Kilimo wameonyesha mahaba makubwa sana kwa wakulima wetu, sekta ya kilimo kwa mwaka huu imetengewa bajeti kubwa haijawahi tokea. Lengo ni kuhakikisha mkulima ananufaika na fursa mbalimba ili kilimo kiwe na tija. Ninaishukuru sana Serikali yetu kwa kupunguza bei yam bole na kutoa ruzuku kwenye bidhaa hii”. Alishukru Mhe. Mwassa.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Mwassa alisema Serikali inayoongozwa na Rais Samia, imerejesha kwa Wananchi, mashamba yote makubwa yaliyokuwa yakimilikiwa na watu Binafsi, na kuongeza kuwa Wakulima watapata fursa ya kumili aridhi baada ya kukukabidhiwa mashamba hayo wayamiliki kisheria.
“Mhe Rais Samia, amerudisha mashamba makubwa mikononi mwa Wananchi. Ni jukumu letu sisi viongozi, kuhakikisha mashamba hayo yanagawiwa vyema ili kila Mwananchi wa Mkoa wa Morogoro apate fursa ya kumiliki Ardhi”. Aliagiza Mkuu huyo wa Mkoa.
Akizungumzia kuhusu skimu za Umwagiliaji, Mhe. Mwassa alisema Serikali imetoa kiasi cha Shilingi 16.5 milioni, kwa Mkoa wa Morogo, za ujenzi na uboreshaji wa miundombinu kwenye skimu tatu za umwagiliaji ikiwa ni mikakati madhubuti ya Serikali katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabia Nchi.
Hitimisho la Wiki ya kilimo Marathoni ilitanguliwa na mashindano yambio yakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Mwassa, Wakuu wa Wilaya pamoja na Wadau mbalimbali. Ambapo mbio hizo ziligawanywa katika umbali tofauti tofauti ikiwepo wa KM 5, Km 10, Km 15 na Km 20.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa