Viongozi wa Serikali Wilayani Gairo wameswa kuacha mara moja tabia ya marumbano na kubisnaha hadharani mbele ya Wananchi na watendaji wa umma, kwani kufanya hivyo ni kujishushia hadhi katika jamii wanayo iongoza na kuleta sifa mbaya na aibu kwao.
Rai hiyo imetolewa na mwenyeiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Gairo, Mheshimiwa Shabani Sajilo wakati wa kikao cha Kawaida cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Juni 10, 2021
“Hii ni aibu sana kwa vingozi wenye heshima kwenye jamii kurumbana na kubishana hadharani namna hii, mna kitia doa Chama tawala (CCM) na mnaji aibisha ninyi wenyewe mbele ya hadhara ya mnao waongoza”, alisem
Alibainisha kuwa kuwepo kwa mgongano wa mawazo na kupishana msimamo ni jambo la kawaida na ndiyo chachu ya maendeleo na kuongeza kuwa kupishana mitazamo na hoja huleta changamoto katika kushughulikia kero za Wananchi kwa kuunganisha ni mawazo ya wengi.
“Nimelazimika kusimama na kusema haya ndugu viongozi wenzangu maana ninaona mwelekeo wa upepo ulivyo hivi sasa jahazi linaweza kuzama kwa kupigwa na mawimbi ya namna hii, nina waasa tuheshimiane na kila mmoja atimize wajibu wake. Muhimu ni kuunganisha tofauti zetu za kimitazamo na mawazo ili zitumike kama fursa bora za kutatua kero za Wananchi wetu”. Alisistiza.
Akaongeza “Mahala pekee ambapo tunapata fursa ya kubishana, kurumbana na kukosoana ni ndani ya chama kupitia vikao vyetu ambavyo hufanyika kwa mujibu wa Katiba ya Chama chetu kikiwepo kikao cha Kamati ya Siasa Wilaya, huko ndiyo mahali sahihi lakini siyo hadharani namna hii”.
Aidha amewataka viongozi hao kutokimbilia kuzungumza madhaifu ya Wilaya kwenye vyombo vya habari kwani kwa kufanya hivyo kuna dunisha kasi ya uwekezaji katika nyanj za utalii, biashara na kilimo hasa kwa wawekezaji wanje wanao tamani kuja kuwekeza Wilayani Gairo.
“Kuongea madhaifu ya ndani kwako kwa majirani au kwenye vyombo vya habari ni kujidharirisha na kujivua nguo pasipokujua kuwa ni kuwapa fursa maadui zako kukuvuruga zaidi, hili nalo si sawa, ni vyema mambo mengine yakafanyika kimya kimya bila kuyaanika kwenye vyombo vya habari ili kuondoa taharuki kwa wengine”, alitanabahisha.
Kikao hicho cha Baraza la Madiwani kilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe, akiongozana na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, wataalamu mbali mbali, watumishi wa Halmashauri na Taasisi nyingine za Umma, viongozi wa Dini, Vyama vya Siasa na Wananchi wa kawaida.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa