Na. Cosmas Mathias Njingo
GAIRO, Morogoro
Nov. 29.2022
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Bi. Msifwaki Haule, ameiomba Serikali, kupitia Wizara ya Kilimo, kuisaidia Halmashauri hiyo kufanya tafiti na upembuzi yakinifu juu ya uchimbaji wa mabawa ili kuwezesha kilimo cha umwagiliaji ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia Nchi.
Bi.Haule ametoa ombi hilo mbele ya Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Peter Mavunde (MB), wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki la Kilimo Gairo, lililohitimishwa kwenye kata ya Rubeho Oktoba 29.2022.
“Mhe. Naibu Waziri mabadiliko ya tabia Nchi yameleta athari kubwa kwa wakulima na kupunguza uzalishaji kutokana na ukame ambao umeikumba Wilaya yetu, kilimo chetu kinategemea mvua za msimu kwa kiasi kikubwa. Tunaiomba Wizara yako kusaidia katika kufanya utafiti wa uchimbaji wa mabwawa ili kuwezesha kilimo cha umwagiliaji”. Aliomba Kaimu Mkuirugenzi huyo.
Bi. Haule aliongeza kuwa kupitia tafiti hizo Halmashauri itabaini njia mbadala za kuendeleza kilimo kwa njia ya umwagiliaji, hali ambayo alieleza kuwa itaongeza uzalishaji wa mazao yenye tija, sambamba kuinua pato la wakulima na wafugaji.
“Kwa kufanya hivyo Mhe. Naibu Waziri, tafiti zitatuonyesha ni namna gani tunaweza tukatumia mabwawa hayo kuwekeza zaidi kwenye kilimo cha Umwagiliaji ili kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao na kusaidia kuinua pato la mkulima badala ya kuendelea kutegemea mvua za asili ambazo hazina uhakika sana, kutokana na mabadiliko ya tabia Nchi ambayo yameleta athari kubwa katika sekta ya kilimo”. Alifafanua Kaimu Mkurugenzi Bi. Haule.
Akihutubia mamia ya wakati wa Kata ya Rubeho walioshiriki kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki la Kilimo, Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe. Mavunde alisema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan imetenga kiasi cha shilingi Bil 400 kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji ambazo zimeelekezwa kwenye uchimbaji wa mabwawa na ujenzi maiundombinu muhimu katika mabwawa hayo.
“Bajeti ya Wizara ya kilimo imeongezeka kutoka Shilingi Bil.294 mwaka 2021/2022 na kufikia kiasi cha shilingi Bil.954 kwa mwaka wa fedha 2022/2023. Ambapo kati ya fedha hizo, kiasi cha shilingi nilioni mia nne zimelekezwa katika uchimbaji wa mabwawa na ujenzi wa miundombinu yote muhimu katika mabwawa hayo”. Asliesma Mhe. Mavunde.
Akaongeza kuwa dhamira ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha uzalishaji unaongezeka na kuwa wenye tija pamoja na kuwawezesha wakulima kuzalisha mara mbili kwa mwaka badala ya kuendelea kuzalisha mazao hafifu kwa kutegemea msimu wa mvua ambao ni mara mojwa kwa mwaka.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame akimkaribisha Mhe. Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde alisema, Wilaya ya Gairo imeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha inatatua kero zinazowakabili wakulima na wafugaji ili dhamiria ya Mhe. Rais Samia ya kuleta mageuzi kwenye Sekta ya Kilimo ifikiwa.
Maadhimisho ya Wiki la Mkulima Wilaya ya Gairo, yalizindiliwa rasmi Oktoba 27.2022, na Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Jabiri Omari Makame, katika kata ya Ukwamani na kuhitimishwa Oktoba 29, 2022, ambapo Shughuli za maonesho ya bidhaa mbalimbali na teeknolojia za kilimo ziliendelea kufanyika na kuwapa fursa Wakulima kutembelea kwenye mabanda ya wadau wakilimo kujifunza ma kujionea shughuli zinazotekelezwa na Wadau hao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa