“KWA KWELI TASAF imenifanyia mambo makubwa sana katika maisha yangu, sitokuja kuisahau kamwe. Mara ya kwanza Nilipokea pesa jumla ya Shilingi 78,000 kwa mkupuo, malipo ya miezi mitatu, yaani elfu ishirini na sita (26,000) kila mwezi, nikaamua kuziwekeza kwenye kilimo cha karanga na mtama”
Mnufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini -TASAF, Christina Simon Samson, akionesha miradi anayoitekeleza ikiwa ni matokeo ya matumzi sahii ya fedha za ruzuku ya Wanufaika wa Mpango wa kunusuru Kaya Maskini TASAF Vitengo anavyouza kwa mkopo. (Picha Na, COSMAS M.NJINGO-GAIRO)
Na. Cosmas Mathias Njingo.
GAIRO, Morogoro.
Ni kauli ya Bi. Christina Simon Samson, Mkazi wa Kitongoji cha Mamuli, Kata ya Gairo, Wilaya ya Gairo, akishuhudia namna ambavyo Mfuko wa Taifa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini III, ulivyo muwezesha kupata mafanikio makubwa kiuchumi na kuondokana na umaskini.
Moja ya Gari, aina ya NOAH inayomilikiwa naBi. Mnufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini -TASAF, Christina Simon Samson (Picha Na. Cosmas Mathias NJingo-GAIRO)
Bi. Christina (41) Mama wa watoto 3 (Me 2 na Ke 1) ni Mnufaika wa moja kwa moja wa Mpango huu wa Kunusuru kaya Maskini III, lakini pia ni mwanakikundi wa Kikundi cha Walengwa wa TASAF cha Upendo, kilichopo katika Kitongoji cha Mamuli Kata ya Gairo.
Anasema kabla ya kuingia kwenye Mpango huu, hali yake kimaisha ilikuwa duni sana, na kwamba familia ilimuelemea kutokana na mahitaji kuwa makubwa tofauti na uwezo wake wa kipato kwa wakati huo, hali ambayo ilimuwia vigumu kukidhi mahitaji muhimu ya kifamilia ikiwepo upatikanani duni wa chakula na fedha za kujikimu na kushindwa kugharamia mahitaji ya shule kwa ajili ya watoto wake.
“Yaani hapo awali niliishi maisha magumu sana, haikuwa kazi rahisi kwangu kuweza kutimimiza mahitaji ya kila siku ya familia, pamoja na mahitaji ya shule kwa wakati huo maana wanangu watatu wote walikuwa wakisoma. Lakini mie leo nimekuwa mtu wa tofauti sana, hali yangu ya maisha imebadilika kwa shilingi elfu ishirini na sita tu za TASAF”. Alibainisha Bi. Christina.
Bi. Mnufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini -TASAF, Christina Simon Samson, akionyesha Vitengo anavyouza kwa mkopo.(Picha Na, COSMAS M.NJINGO-GAIRO)
Mlengwa huyo wa TASSAF anasimulia kuwa baada ya kupokea fedha hizo, aliona ni vema bora kuwekeza katika kilimo cha zao la Mtama na Karanga, ambapo anasema aliweza kulima ekari tano (05) za kilimo mseto; na kufanikiwa kuvuna jumla ya magunia 42, kati ya hayo 26 ya karanga na 16 ya mtama.
“Niliwekeza kwenye kilimo mseto ekari tano za Mtama na Karanga, nikavuna gunia 26 za karanga na Mtama gunia 16, nikahifadhi gharanai kusubiri bei ya soko ipande. Baada ya Bei ya Karanga na Mtama kuwa juu nikaamua kuuza na kufanikiwa kupata kiasi cha Shilingi Milioni moja na Laki moja (1,100,000)”. Akafafanua.
Anasimulia zaidi kwamba alitoa kiasi cha Sh.800, 000 (laki nane) katika pesa alizopata baada ya kuuza mtama na karanga, akanunua pikipiki iliyokwisha tumika na kuanzisha biashara ya kusafirisha abiria maarufu Boda bodam, kazi ambayo ilidumu kwa kipindi cha miezi 7, pesa alizosikusnya akanunua tena pikipiki nyingine. Hivyo kumiliki pikipiki mbili za kufanyia biashara ya kusafirisha abiiria (boda boda)
Bi. Chritina anabainisha kuwa hakuishi hapo kwani kupitia biashara hiyo ya boda boda aliuza pikipiki moja akaongezea pesa na kununu gari aina ya Noah (iliyotumika), ambayo inafanya kazi ya kubeba abiria na mizigo kwenda minadani maeneo mbalimbali ndani nan je ya Wilaya ya Gairo.
Anasema “Baadae nilikutana na Mtu mmoja anauza gair yake aina ya Noah kwa shilingi milioni nne. Nikaona hiyo kwangu ni fursa nzuri hivyo nikauza pikipiki moja nikaopngezea pesa katika akiba niliyokuwa nayo nikaichukua ile Noah. Nimeifanya kama daladala ya kubeba Wafanyabishara wa minadani”.
Pamoja na changamoto za hapa na pale Bi. Christina anaeleza kuwa hazimkatishi tamaa, na kwamba anendelea kupambana usiku na mchana ambapo hadi sasa anamiliki Noah mbili, zote zinabeba abiria (wafanya biashara) kuzunguka magulio na minada mbalimbali Wilaya za Gairo na Mvomero, na Wilaya jirani za Mkoa wa Dodoma, Manyara na Tanga.
Kuhusu mabadiliko ya kiwango cha pesa za Ruzuku ya Wanufaika wa kaya maskini anachopokea kwa mwezi, Bi. Christina, anaeleza kuwa hapo awali alikuwa akipokea kiasi cha shilingi 26,000 na hivi sasa anapokea jumla ya shilingi 34,000 kwa mwezi, hali ambayo anasema imemsaidia kuanzisha biashara nyingine ya kuuza vitenge kwa njia ya mkopo ambavyo hununua kutoka nchini Malawi na vingine hapa hapa Nchini.
“Zamani nilikuwa napokea shilingi 26,000, ila naishukuru Serikali imeniongezea kwa sasa ninapokea Sh.34, 000, ambazo zimeniwezesha kuongeza biashara nyingine ya kuuza vitenge kwa njia ya mkopo. Vitenge hivi nanunua kutoka viwanda vya hapa nchini na vingine naagiza Malawi”. Alifafanua Bi. Christina.
Akaongeza kuwa bei ya vitenge hivyo huuza kwa shilingi 28,000 kwa vitenge vya Tanzania, na Shilingi 35,000 kwa vitenge vya Malawi, na kwamba huuza kwa fedha taslimu na mkopo wa mwezi mmoja
Kupitia shughuli hizo za ujasiliamali zilizotokana na uwekezaji wa Mtaji wa mdogo wa Sh. 26,000 za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini TASSAF, Bi. Christina ameweza kutengeneza ajira kwa vijana waendesha Boda Boda ikiwepo watoto wake wawili wa kiume ambao ndiyo madera wa Noah zinazofanya safari kwenye magulio na minada mbalimbali.
Je, anaushauri gani kwa Wanawake wenzako ambao ni Wanufaika wa TASSAF lakini bado hawajaona fursa za kuwasaidia kuinuka kiuchumi? Bi. Christina anawaasa Wanawake wenzake wasidharau pesa za ruzuku wanazopata za Mpango wa TASAF, badala yake watumie fedha hizo kuwekeza kwenye fursa mbalimbali zilizopo katika maneo wanayoishi ili kupunguza Umaskini.
Kwa upande mwingine anaishauri Serikali kuongeza kiwango cha Ruzuku kwa Wanufaika waMpango wa TASAF ili kuwezesha kukabiliana na hali ya maisha ya sasa inayochagizwa na mfumuko wa bezi za bidhaa na huduma mbalimbali kwani uhitaji bado ni mkubwa.
“Umaskini bado upo miongoni mwa jamii, na uhitaji ni mkubwa sana, hivyo ushauri wangu kwa Serikali inayoongozwa na Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iangalie na kufanyama maboresho ya kiwango cha fedha inayotoa kwa sasa. Hali ya maisha imekuwa ngumu sana kutokana na kupanda kwa bei ya bidhaa na huduma mbalimbali za kijamii”. Alisisitiza Mnufaika huyo wa TASAF.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa