Na. Cosmas Mathias Njingo. GAIRO
Agosti 19.2023Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Bi. Sharifa Nabalang'anya; amewaomba Waheshimiwa Madiwani kufanya kazi kwa ushirikiano na Maafisa ugani ngazi za vijiji na Kata ili kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao.
Ametoa wito huo katika Kikao cha Baraza la Wahe. Madiwani cha kujadili Taarifa za Robo ya Nne za utekelezaji kwa mwaka wa fedha ulioishawa 2022/2023 kilichofanyika Agosti 11.2023 katika Ukumbi mkubwa wa mikutano wa Halmashauri.
“Niwaombe Wahe. Madiwani mshirikiane na Wataalam wetu wa Ugani waliopo katika Vijiji na Kata zenu, hii itasaidia sana kuimarisha utendaji na kuongeza uwajibikaji hasa katika kuwafikia wakulima kwa na kutatua changamoto zao”. Alisema Bi. Nabalang’anya.
Alisema Wahe. Madiwani wanwajibu mkubwa wa kusimamia wataamba waliopo katika kata zao ili malengo ya serikali yatime, sambamba na kuhakikisha vitendea kazi walivyopewa Maafisa ugani hao ikiwepo pikipiki; zinatumika kwa usahihi ili kuleta tija kwa wakulima katika kuongeza uzalishaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa