Na. Cosmas Mathias Njingo. GAIRO
Agosti 13.2023
“Tuendelee kuishi kwa amani, tuishi kwa upendo na kuimarisha umoja wetu. Kwa sababu kinacho tuunganisha sisi ni kitu kimoja Utanzania wetu; Tanzaiania ni moja tu hatuna Nchi nyingine”. Kauli ya Mhe Jabiri Omari Makame Mkuu wa Wilaya ya Gairo
Alitoa wito huo wa kuimarisha umoja, mshikamano na kuishi kwa Amani alipokuwa akizungumza na baadhi ya viongozi wa Kitongoji cha Kunkresha kijiji cha Kitaita Kata ya Leshata Wilaya ya Gairo na Kitongoji cha Matilei kilichopo Wilaya ya Kilindi wakati wa ziara yake kubaini hali ya migogoro ya ardhi na mipaka kati ya vijiji na vijiji pamoja na Wilaya na Wilaya.
Makame alisema kila Mtanzania anayohaki ya kuishi na kufanya shughuli za kiuchumi mahala popote ndai na nje ya Mkoa au wilaya yake ya asili kwakuwa Tanzania ni moja imebarikiwa tunu mbalimbali ikiwepo ya Amani, mshikamano, umoja na upendo baina ya Wananchi wake.
“Hatupaswi kuishi kwa kubaguana kwa misingi ya makabila yetu ambayo hayawei kutuetea maendeleo na kumarisha usalama wetu. Kwa hiyo ndugu zangu ninaomba mtambue kuwa kinacho tuunganisha na kutuletea maendeleo ni Mshikamano, upendo, Umoja na Zaidi sana Amani tuliyonayo ni lazima kuhakikisha tunailinda” alisisitiza Mhe. Makame.
Mkuu huyo wa Wilaya akasisitiza migogoro yote ya mipaka na migogoro ya ardhi hana budi kukomeshwa ndani ya Wilaya ya Gairo kwani ikiendelea inaleta udumavu wa fikra na kupunguza kasi ya kukua kwa manedeleo ya mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa