Na. Cosmas Mathias Njingo, DAR ES SALAAM.
Juni 21.2024
Maafisa Habari, Mawasiliano na Itifaki wa Serikali wametakiwa kutumia ujuzi walioupata kupitia mafunzo ya mada mbalimbali zilizotolewa wakati wa kikao kazi cha 19 cha Maafisa Habari wa Serikali, kilichofanyika Jijini Dar es salaam.
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Mawasilino na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (MB), akifunga kikao kazi hicho kilichofanyika Juni 21 na 22. 2024, katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City.
“Niwaombe Maafisa Mawasiliano na Itifaki wa Serikali, twende tukatumie vizuri ujuzi tulioupata katika kikao kazi hiki kuboresha utendaji kazi wetu. Ujuzi huu utakuwa na maana sana kwetu, ikiwa tutaona mabadiliko kwenye namna tunavyofanya kazi” alisisitiza Mhe.Nauye.
Aidha Mhe. Nape amemwagiza Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Habari Maelezo, kuhakikisha anaweka utaratibu wa kuendesha mafunzo kwa Maafisa Habari wa Serikali katika Kanda zao, ili kuwajengea uwezo wa kuboresha utendaji wao wa kazi wa kila siku, badala ya kusubiri utaratibu wa sasa wa kufanya mafunzo mara moja kwa mwaka kupitia vikao kazi.
“Hii ya kufanya mafunzo mwaka hadi mwaka wakati wa kikao kazi kama hivi nadhani si sawa. Nimemwagiza Mkurugenzi wa Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali, kuandaa utaratibu wa kuendesha mafunzo ya Kikanda kwa Maafisa Habari wa Serikali, na kila mwezi nipate mrejesho.” Alisema Waziri huyo wa Habari.
Kikao kazi hicho ka 19, kilihitimishwa rasmi na Mhe. Nape Nauye Juni 21.2024, ambapo zaidi ya Maafisa Habari, Mawasilino na Ifaki wa Serikalini 500 walikutana kutoka Wizara, Taasisi za Umma na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Katika kuhitimisha Kikaokazihicho Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, ilitoa tuzo mbalimbali ikiwepo Vikombe na Vyeti kwa Wizara, Taasisi na Halmashauri zilizofanya vizuri kwenye eneola utoaji Habari na Mrejesho wa Wananchi kupitia Vitengo vya Mawasiliano Serikalini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa