Na. Cosmas Mathias Njingo
Juni 7.2023
1. Hakuna mahali ambapo Serikali imekubaliana kuuza bandari ya Dar es Salaam na mtu akibisha mwambieni alete ushahidi
2. Kilichotangazwa na Bunge ni kukaribisha maoni ya wadau kabla Bunge halijaridhia mkataba wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai
3. Dhamira ya Serikali ninkuongeza ufanisi wa Bandari zetu. Mfano bandari ya Dar es Salaam tutoke kwenye kuhudumia shehena ya tani Milioni 18 twende kwenye zaidi ya tani Milioni 50, Meli zipunguze kusubiri kushusha mizigo kutoka wastani wa siku 9 za sasa hadi chini ya siku moja( actually 2hrs)
4. Tuiwezeshe bandari yetu kuhudumia ipasavyo reli yetu ya SGR ambayo ina uwezo mkubwa ya kufunga treni ya kubeba hata zaidi ya tani 10,000 kwa wakati mmoja. Tukibaki na hali ilivyo sasa bandari yetu haina uwezo huo
5. Kupunguza gharama za bandari na kupunguza gharama za bidhaa zinazopita bandari ya Dar.
6. Tunaikaribisha sekta binafsi ili pesa za Serikali tuzielekeze kwenye huduma za kijamii afya, elimu, barabara, dawa nk. Uboreshaji wa bandari unahitaji pesa nyingi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa