Na. Cosmas Mathias Njingo
GAIRO, Morogoro
Novemba 4.2022
Utekelezaji wa ujenzi wa kituo Cha Afya Tarafa ya Nongwe umefikia tamati ambapo kituo hicho kinatarajiwa kuanza kutoa huduma mara baada ya taratibu nyingine kukamilika.
Ujenzi huo umegharimu kiasi cha Sh. 500,000,000 za fedha za tozo ya miamala ya Simu.
Utekelezaji wa ujenzi wa kituo cha Afya Nongwe, umehusisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa Nje (OPD), maabara, Wodi ya Wazazi na jengo la upasuaje wanawake.
Kukamilika Kwa majengo hayo ni mwarobaini wa tatizo la upatikanaji wa huduma za Afya kwa Wakazi wa Tarafa ya Nongwe, pamoja na kuokoa maisha ya wajawazito
Jengo la wagonjwa wa Nje (OPD) kituo cha afya Nongwe, Kata ya Nongwe Tarafa ya Nongwe
Sehemu ya ndani ya jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD) Kituo cha Afya Nongwe
Jengo la Maabara Kituo cha Afya Nongwe
Jengo la Upasuaji na WODI ya Wazazi kituo cha Afya Nongwe
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa