"Baraza la Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo linaunga mkono na kutoa baraka zake zote swala la utaratibu mpya wa uuzaji wa mazao. Utaratibu huu ni mzuri na utaondoa kabisa changamoto ya Wafanyabiashara wakubwa kuwagalaliza Wakulima kwa kununua mazao kwa bei ya chini. Ni vizuri sasa Elimu hii ipelekwe kwa Wananchi na Wakulima ili nao wajue nia njema ya Serikali yetu ya kuuza mazao kwa utaratibu na kwa vipimo maalum". Mhe Rachel Nyangasi, Mwenyekiti wa Halmashauri
Mhe. Nyangasi alitoa kauli hiyo akichangia hotuba ya Mhe. Jabiri Makame, Mkuu wa Wilaya ya Gairo wakati akitoa salam za Serikali kwa Wahe.Madiwani katika Mkutano wa Baraza la kawaida wa taarifa za robo ya tatu kipindi cha Januari-Machi 2023/2024, uliofanyika kwenye ukumbi mkubwa wa Mikutano wa Halmashauri
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa