Na. Cosmas Mathias Njingo. GAIRO
Agosti 12.2023
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Makame amewaagiza Katibu Tawala Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kupitia Divisheni ya Ardhi na Mipango miji kuandaa ratiba ya kutembea kwenye kata na vijiji vyenye migogoro ya ardhi ili kutatua migogoro hiyo haraka.
Ametoa agizo hilo hivi karibuni alipofanya ziara ya kuona hali ya mgogo wa mipaka kati ya Wilaya ya Gairo na Wilaya ya Kiteto Mkoa wa Manyara na Kitongoji cha Matilei kilichopo Wilaya ya Kilindi Mkoa wa Tanga, katika kijiji cha Kitaita kitongoji cha Kinkuresha kilichopo kata ya Leshata Wilayani Gairo.
“Nawaagiza Katibu Tawala kwa kushiriiana na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kukaa pamoja na kupanga ratiba ya kutembelea Kata na Vijiji vyote vyenye migogoro ya mipaka na Ardhi ili kuona namna ya kutatua migogoro hiyo haraka iwezekanavyo.” Aliagiza Mhe. Makame
Amesema migogoro inakuwa sugu inasababisha shughuli nyingi za maendeleo kukwama hali ambayo inawanyima fursa wananchi katika maeno husika kunufaika na shughuli mbalimba za miradi ya maeneleo inayoletwa na Serikali sambamba na kuwanyima fursa muhimu ya kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji, Kata na Taifa kwa ujumla.
Makame alisema migogoro yote inayohusu mpaka inapaswa kushughilikwa hara iwezekanavyo kabla ya kuingia kwenye uchaguzi wa Viongozi Serikali za Mitaa mwaka 2024 na Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakao fanyika mwaka 2025.
“Migogoro inapozidi inaleta athari kubwa sana kwenye shughuli za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, lakini pia inaathiri chaguzi za viongozi kwa ngazi za Serikali za Mitaa na uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Waheshimiwa Madiwani”. Alifafanua.
Kwa upande mwingiNE Mhe. Makame amewataka Katibu Tawala Wilaya na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kuandika barua kwenda kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro ya kukumbushia hatua zilizofikiwa za utatuzi wa mgogoro wa mpaka baina ya Wilaya ya Gairo Mkao wa Morogoro na Wilaya ya Kiteto Mkoa wa Manyara ili kupata ufumbuzi wa haraka wa mgogoro huo mapema kabla ya chaguzi zijazo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa