Imeelezwa kuwa hadi kufikia Agosti 4, 2021 Wilaya ya Gairo imeripotiwa kuwa na wahisiwa wa UVIKO walio fika kupatiwa huduma Kituo cha Afya Gairo ni watano ambao wamelezwa wodini wakiendelea kupata huduma za kitabibu.
Hayo yalisemwa na Katibu Tawala Wilaya ya Gairo Bwana Augustino Chazua akitoa hotuba ya uzinduzi wa Chanjo ya UVIKO kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Hiyo Mheshimiwa Jabir Omari Makame, uliofanyika katika kituo cha Afya Gairo Augusti 4 2021 na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali ikiwepo Wananchi.
Chazua aliwambia Wanachi hao kuwa vurusi vya UVIKO vinasambaa kwa kazi kubwa na kuathiri watu wengi kwa muda mfupi na kuwasihi kuchukua tahadhari muhimu kama wanavyo elekezwa na wataalamu wa tiba.
“Ndugu zangu nawakumbusha kuwa makini na kujilinda nyakati zote, ni muhimu kuzingatia maelekezo ya wataalu wetu wa Afya kila mara wanatukumbusha kuchukua tahadhari kwa kuhakikisha tunatumia barakoa kwa usahihi, kunawa miko kwa maji tiririka na sabau sambamba na kutokumbatiana au kusalimiana kwa kushikana mikono”. Aliwaasa.
Alifafanua kuwa Serikali ya Tanzania ilizindua matumizi ya chanjo ya UVIKO nchini mnamo Julai 282021 baada ya kuwepo kwa milipuko ya ugonjwa wa huu Duniani kote, na kwamba kumeingia wimbi la tatu la virusi vinavyoshambulia kwa kasi mfumo wa upumuaji wa mwanadamu.
Wakati Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), likiripoti jumla ya kesi 186,411,011 zilizothibitishwa za wagonjwa wa UVIKO-19 pamoja na Vifo 4,031,725 kufikia hadi Julai 12, 2021, ulimwenguni kote, Nchini Tanzania kumekua na kesi 1,017 za maambukizi hayo huku waliopona ni 183 wakati vifo vinaripotiwa kufikia watu 21 hadi mpaka tarehe 2 Agosti 2021.
Imebainishwa kuwa ugonjwa wa UVIKO umekuwa tishio katika ukuaji wa Ustawi wa jamii na kwa kiasi kikubwa nchi zote ulimwenguni kiafya, kiuchumi na kijamii huku Tanzania ikitajwa kuwa miongoni mwa Nchi zilizo athiriwa kwa kiasi kikubwa Barani Afrika.
Hata hiovyo katika kupambana na janga hili Tanzania kupitia Wizara ya Afya, Jinisa, Wanawake, Watoto na Wazee imetekeleza mikakati na jitihada mbalimbali za kudhibiti janga hili ikiwa ni pamoja kutoa elimu kwa Umma juu ya njia za kudhibiti na kuzuia maambukizi (IPC.
Njia hizo ni pamoja na kukaa mbalimbali mita moja kati ya mtu na mtu, Uvaaji wa barakoa, unawaji wa mikono kwa sabuni na maji tiririka sambamba na kuepuka mikusanyiko.
Aidha, kwa upande mweingine Serikali inachukulia chanjo ya UVIKO kuwa njia moja wapo ya kudhibiti magonjwa huku chanjo hiyo ikitajwa kuwa ni njia bora ya kupunguza kasi ya maamukizi ya virusi vinavyo ambuliza ugonjwa huo kwani inapunguza ukali wa dalili, kuugua na kupunguza vifo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa