• Mawasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
GAIRO DISTRICT COUNCIL
GAIRO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Authorities Halmashauri ya Wilaya ya Gairo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dira
    • Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni za Halmashauri
      • Seksheni ya Rasilimali Watu
      • Seksheni ya Utawala
    • Divisheni ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Baraza la Madiwani
  • Miradi
    • Miradi ya Maendeleo
      • Sekta ya Elimu Msingi
        • Miradi Mipya
        • Miradi iliyokamilika
      • Sekta ya Elimu Sekondari
      • Sekta ya Afya
      • Sekta ya Barabara/Miundombinu
      • Sekta ya Maji
  • Machapisho
    • Katiba ya JMT
    • Sheria ndogo ndogo za Halmashauri
    • Hotuba Mbalimbali
    • Sera ya Elimu
    • Taarifa za Hesabu za Mwisho
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

WANAOISHI NA ULEMAVU, WAASWA KUTOJITENGA NA JAMII INAYOWAZUNGUKA

Posted on: December 3rd, 2022

Na. Cosmas Mathias Njingo

GAIRO, Morogoro.

Disemba 3.2022.

Wito umetolewa kwa Watu wanaoishi na hali ya Ulemavu, kuacha kujiona wanyonge sambamba na kuepuka vitendo vya kujinyanyapaa wao wenyewe miongoni kawani kwa kufanya hivyo kunawakosesha kushiriki katika shughuli za kujipatia riziki na kukosa fursa mbalimbali za kuwakawmua kiuchumi na kijamii kwa ujumla

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Clement Msulwa (Diwani Iyogwe) akizungumza na watu wanaoishi an Ulemavu (hawapo pichani) katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Watu wanaoishi na Ulemavu yaliyoadhimishwa Kiwilaya Katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Disemba 3.2023: PICHA NA COSMAS M. NJINGO

Rai hiyo imetolewa na Makama wa Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Clement Msulwa (DIWANI-IYOGWE) wakati akitoa salam za Halmashauri kwa niaba ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe.Rahel Nyangasi (Diwani kata ya Chigela) wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulamavu ambayo huadhimishwa tarehe 3 Disemba duniani kote.

Moja wa Watu wanaoishi na Ulemavu wa Ngozi akihudhuria kilele cha maadhimisho ya Sherehe za watu waishio na Ulamavu Wilayani Gairo

“Hakuna mtu anayependa kuzaliwa wakiwa na hali hiyo, lakini pia hakuna mtu anayependa atoke kwenye ujana kwenda rika la utu uzima na uzee akiwa melamavu. Ulemavu unaweza kumpata Mtu yoyote wakati wowote na popote. Hivyo ninyi ambao mpo katika hali hii, msijisikie unyonge na kujiona mpo peke yenu, wala msijione mmetengwa na jamii au Serikali”Alsema Mhe. Msulwa.

Afisa Uatawi wa Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Bi. Tatu Nkango akizungumza na watu waioshio na Ulemavu

Mhe. Msulwa akasema kuwa Serikali inatambua na kuthamani watu waishio na ulemavu kwa kuwapa fursa mbalimbali za kushiriki katika vyombo vya maamuzi kuanzia ngazi za vijiji hadi Taifa pamoja na kuwawezesha kupata mitaji ya kuendesha shuguli za uzalishaji mali ili kujikwamua kiuchumi kupitia mikopo ya asilimia 2, inayotolewa na Halmashauri kutokana na Makusanyo ya mapato ya ndani kwa ajili ya vikundi vya Watu wenye Ulemavu.

“Ndiyo maana Serikali imepanga na kuelekeza Halmashauri zote nchini kutenga asilimia 10 kwa ajili ya vikundi vya Vijana, Wanawake na Watu Wenye Ulemavu, lengo ikiwa nikuhakikisha makundi haya yananufaika ili kujikwamua kiuchumi na kuondokana hali ya utegemezi” alifafanua Makamu Mwenyekiti huyo.

Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabir Makame (mwenye kofia) akigawa msaada wa sabuni na mafuta kwa watu waishio na ulemavu

Alibainisha kuwa kundi la Watu wenye Ulemavu limetengewa asilimia mbili (02%) ya fedha za makusanyo ya mapato ya ndabi ya Halmashauri huku Kudndi la Wanawake na Vijana yakipata asilimia nne (04%) kila moja, ambazo zinalenga kuwainua kiuchumi na kuboresha maisha yao.

Mkalimani wa lugha ya ishara akisaidia kutafasiri yale yanayosemwa na viongozi kwa ajili ya kuwasaidia wenye ulemavu wa kusikia (viziwi)

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Bi. Msifwaki Haule amewataka Watu wanaoishi na Ulemavu Wilayani humo kuwa milango ipo wazi endapo wanapata changamoto yoyote anawakaribisha ili kujadiliana na kutafuta njia bora za kutatua changamoto hiz.

Awali Mwenyekiti wa Jumuia ya Watu wenye Ulemavu Wilaya ya Gairo Bw. Dickson Andrea Msagala akisoma risala kwa Mgeni Rasmi, alisema Jumuia ya Walemavu imetekeleza maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na Mhe. Jabiri Omari Makame Mkuu wa Wilaya ya Gairo ikiwepo kuitaka jumuiya hiyo kufanya uchaguzi ili kupata viongozi wa nyadhifa mbalimbali watakao wawakilisha katika kusimamia na kutekeleza majumu mbalimbali kwa maslahi mapana ya Watu waishio na Ulemavu.

Mwenyekiti wa Jumuia ya Watu wenye Ulemavu Wilaya ya Gairo Bw. Dickson Andrea Msagala.

Matangazo ya Kawaida

  • Orodha ya Wanafunzi Waliochaguliwa kujiunga na Shule za Sekondari za Gairo December 16, 2022
  • SOMA TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KADA MBALIMBALI May 25, 2022
  • TANGAZO LA ZABUNI YA KUZOA TAKA, KUFANYA USAFI NA KUKUSANYA USHURU WA USAFI June 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI July 19, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MIKAKATI YA SERIKALI KATIKA KUDHIBITI MAGONJWA YA MILIPUKO

    December 16, 2022
  • KAIRUKI: SIMAMIENI ZOEZI LA UCHUNGUZI WA AWALI WA WATOTO

    December 12, 2022
  • WATOA HUDUMA YA VYAKULA WATAKIWA KUPIMA AFYA KUFIKIA TAREHE 31 DISEMBA 2022.

    December 09, 2022
  • MADIWANI WATAKIWA KUSIMAMIA UKUSAJI MAPATO, KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO NA WATENDAJI WA KATA

    December 08, 2022
  • Tazama zote

Video

VIBE LA MAKARANI WA SENSA GAIRO
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Zabuni za Manunuzi
  • Zabuni za Ujenzi
  • Huduma

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Tanzania
  • GAIRO ONLINE TV
  • MATOKEO YA MTIHANI WA TAIFA KIDATO CHA SITA 2022 GAIRO SEKONDARI
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Mawasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.

    Sanduku la Posta: 40, GAIRO

    Simu ya Mezani: +255232935454

    Simu ya Kiganjani: +255 767498981

    Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa