Na. Cosmas Mathias Njingo
GAIRO, Morogoro.
Oktoba 6. 2022
Wananchi wengi hususani wanawake waishio vijijini, wamehamasika kwa kiwango kikubwa juu ya mpango wa Serikali wa kukuza sekta isiyo rasmi ya kifedha na kuhakikisha wanajiunga kwenye vikundi na kufaidika na fursa za kujiwekea akiba na kupata mitaji kwa ajili ya shughuli za kiuchumi.
Viongozo wa Kijiji cha Ikwamba katika picha ya pamoja wa viongozi wa Kikundi cha Jitihada (Picha Na. Cosmas Mathias Njingo)
Katika kudhihirisha hilo kijiji cha Ikwamba, kilichopo kata ya Mandege Tarafa ya Nongwe kinatajwa kuwa miongoni mwa vijiji ambavyo wanawake wake wamehamasika kwa kiwango kikubwa kujiunga na vikundi vya kiuchumi, vya akiba na mikopo. Hii inaonyesha ni kwa naman gani wanawake wamechoshwa na hali ya umaskini uliyokithiri, na kusababisha kuongezeka kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia unaotokana na kuwa tegemezi kwa asilimia kubwa.
Kwa mujibu wa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Ikwamba, Bwn. Kashindye Severine Kassote, Ikwamba inajumla ya vikundi 11 vya Kiuchumi vinavyoundwa na Wanawake pekee, huku kila kikundi kikiwa na wanachama wasiozidi 15 kulingana na masharti yaliyowekwa kuhusu kanuni za uanzishwaji wa vikundi vya kiuchumi vya wanawake.
Kati ya vikundi hivyo 11, 6 tayari vimeingizwa katika kundi la Wanufaika, kupitia mpango wa kunusuru Kaya maskini unaosimamiwa na Serikali kwa asilimia 100, unaotekelezwa kwa Mfuko wa Taifa wa Maendelo ya Jamii (TASAF).
Wanakikundi wa kikundi cha 'UPENDO' Ikwamba shuleni, Kata ya Mandege wakiwa katika bada lao la kufugia kuku wa kienyeji (Picha Na. Cosmas Mathias Njingo-GAIRO)
Vikundi hivyo 6 ambavyo vipo katika kundi la walenga wa mpango wa TASAF kijijini hapo ni pamoja na kikundi cha UPENDO kutoka kitongoji cha Ikwamba Shuleni, kikundi hiki kinajishughulisha na ufugaji wa kuku wa kienyeji. Kupitia mradi huo wa ufugaji, UPENDO imekuza mtaji wake kufikia Sh.1 455, 000 (Milioni moja laki nne na elfu Hamsini na tano) kutoka mtaji wa Sh.37,500.
Wanakikundi wa Kikundi cha NGUVU KAZI, kutoka kata ta Matongo. Kikundi hiki cha kiuchumi kinashughulika na uuzaji wa miwa (Picha Na. Cosmas Mathias Njingo-GAIRO)
Kikundi cha JITAHIDI cha Kitongoji cha Midindo, kinajishughulisha na mradi wa kununua na kuuza mahindi. Kilianza na mtaji wa Sh.35, 000, ambapo kwa sasa thamani ya mtaji wake imeongezeka mara 36 zaidi na kufikia shilingi 1,269,000.
Kikundi cha JITAHIDI, Kitongoji cha Midindo, shughuli kuu ya kiuchumi ni mradi wa kununua na kuuza Mahindi (Picha Na Cosmas Mathias Njingo-GAIRO)
Kikundi cha kikundi NGUVU KAZI cha Kitongoji cha Matongo chenyewe thamani ya mtaji wake kwa sasa ni sh. 1,200,000 kutoka mtaji wa sh.400, 000 ongezeko la mara nne Zaidi katika kipindi cha miezi 10 tu kupitia mradi wa miwa.
Vikundi vingine ni AMANI kilichopo kitongoji cha Msekeni, kinatekeleza mradi wa kukunua na kuuza Maharage, Amani ilianza na mtaji wa Sh.37, 000, na sasa mtaji wake umeongezeka katika kipindi cha meizi 5, kufikia thamani ya Sh.800, 000 (laki nane).
kikundi cha AMANI ‘A’ cha Kitongoji cha Msekeni, kinajishughulisha na Mradi wa kuuza Maharage (Picha na Cosmas Mathias Njingo-GAIRO)
Uwepo wa vikundi vya hivi katika kijiji cha Ikwamba, imekuwa ni chachu katika kuogeza kasi ya uchangia na utekelezaji wa shughuli za maendeloe, na kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi kuanzia ngazi ya famila na jamii nzima kwa ujumla, kwa Wananchi wa Kijiji hapo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa