• Mawasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
GAIRO DISTRICT COUNCIL
GAIRO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Authorities Halmashauri ya Wilaya ya Gairo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dira
    • Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni za Halmashauri
      • Seksheni ya Rasilimali Watu
      • Seksheni ya Utawala
    • Divisheni ya Mipango na Ufuatiliaji
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Baraza la Madiwani
  • Miradi
    • Miradi ya Maendeleo
      • Sekta ya Elimu Msingi
        • Miradi Mipya
        • Miradi iliyokamilika
      • Sekta ya Elimu Sekondari
      • Sekta ya Afya
      • Sekta ya Barabara/Miundombinu
      • Sekta ya Maji
  • Machapisho
    • Katiba ya JMT
    • Sheria ndogo ndogo za Halmashauri
    • Hotuba Mbalimbali
    • Sera ya Elimu
    • Taarifa za Hesabu za Mwisho
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

WATOA HUDUMA YA VYAKULA WATAKIWA KUPIMA AFYA KUFIKIA TAREHE 31 DISEMBA 2022.

Posted on: December 9th, 2022

Cosmas Mathias Njingo; 

Gairo, MOROGORO.

Disemba 9.2022.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mhe. Rahel NYANGASI (Diwani kata ya Chigela) amewaagiza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi. Msifwaki Haule na Afisa Usafi na Mazingira Bw. Alexanda Sanga, kuhakikisha ifikapo Disemba 30.2022 watoa huduma wote wa vyakula wawe wamepima afya zao.

Mhe. Nyangasi ametoa agizo hilo Disemba 8.2022 katika kikao cha Baraza la Waheshimiwa Madiwani, la kujadili taarifa za Robo ya Kwanza kwa kipindi cha Julai-Septemba 2022/2023 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.

“Ninatoa agizo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri na Mtaalamu wake anayesimamia Usafi na Mazingira, kuhakikisha watoa huduma wote wa vyakula katika Wilaya ya Gairo, wawe wamepimwa afya zao, nipewe taarifa za utekelezaji wa Agizo hili baada ya tarehe 30/12/2022”. Aliagiza Mhe. Nyangasi.

Alisema kwa mujibu wa sheria za uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, ambazo zilitungwa na Baraza hilo la Waheshimiwa madiwai miaka kadhaa iliyopita wakati wa mchakato wa uanzishwaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, na kuzipitisha wenyewe ili ziwaongoze katika kusimamia utekelezaji wa shughuli za mamlaka za Serikali za Mitaa.

“Tunachofanya ni kutekeleza matakwa ya sharia ndogo za uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, ambazo mtakumbuka tulizitunga sisi wenyewe Waheshimiwa Madiwani wakati Gairo imepewa hadhi ya kuwa Halmashauri ya Wilaya”. Alifafanua Mwenyekiti Nyangasi.

Watoa huduma za vyakula wanaotajwa katika chanzo hicho na wanaotakiwa kupima afya zao ni pamoja na Mama/Baba Lishe, wachoma mishikaki na chipsi, wauzaji wa vitumbua, maandazi, mikate, wafanyakazi kwenye mashine za kukoboa na kusaga nafaka pamoja na wahudumu wa Migahawani na Mahotelini.

Kizungumzia kuhusu matokeo ya Tahifa ya Mtihani wa kuhitimu elimu ya Msingi, Mwenyekiti Nyangasi alisema Wilaya ya Gairo kwa mwaka huu imeshika nafasi ya mwisho Kimkoa hali ambayo haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa Halmashauri hiyo.

Akitoa salam za Serikali kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Gairo. Mhe. Jabiri Omari Makame, Kaimu Katibu Tawala Wilaya Bi. Annamary Mwamsendwa alisema Mhe. Mkuu wa Wilaya hiyo amesikitishwa na matokea mabaya ya Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba 2022 ambapo Wilaya ya Gairo imeshika nafasi ya mwisho Kimkoa, na kwamba matokeo hayo yatoe dira ya viongozi wote kijutafakari na kuona namna ya kuondokana na hali hiyo.

“Mhe Mkuu wa Wilaya amesikitishwa sana na matokeo ya mtihani wa Taifa wa darasa la saba mwaka huu. Lakini ameagiza tulichukulie swala hili kuwa ni changamoto ya kutafuta mbinu bora za kuongeza ufaulu ili kuondokana na hali hii”. Alisema Bi. Annamary.

Naye Diwani wa kata ya Chakwale Mhe. Ramadhani Kimwaga alisema matokeo hayo mabaya ya Darasa la Saba yanasikitisha na kutia aibu lakini kila mmoja anapaswa kuyapokea katika mtazamo chanya wa kutafuta mahala panapovuja ili kuziba matundu yote na kuleta matokea chanya kwenye mitihani ijayo.

“Mheshimiwa Mwenyekiti kiukweli kabisa matokeo haya ya Mtihani wa Taifa wa Darasa la saba kwa mwaka huu yanaumiza na kutia aibu, lakini ni vyema tuyapokee katika mtazamo chanya ili kila mmoja kwa nafasi yake atimize wajibu wake”. Alisema Mhe. Kimwaga.

Kikao hicho cha Baraza la Waheshimiwa Madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Gairo kilitanguliwa na Kikao cha Baraza la kata kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya Kata kwa kipindi cha Robo ya Kwanza ya Julai Septemba 2022/2023 kilichofanyika Disemba 7.2022.

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO LA KUITWA KWEYE USAILI WAOMBAJI NAFASI ZA AJIRA MTENDAJI WA KIJIJI III NA DEREVA II September 21, 2024
  • TANGAZO LA HALMASHAURI KUKUSANYA USHURU WA USAFI May 07, 2024
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA PROGRAM YA BBT May 18, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA DEREVA July 12, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MAJALIWA AFUNGUA TAWI LA BENKI YA WATU WA ZANZIBAR MKOA WA MOROGORO

    July 17, 2024
  • GAIRO SEKONDARI YATEKELEZA AGIZO LA KULIMA BUSTANI ZA MBOGAMBOGA, MATUNDA

    July 15, 2024
  • MARUFUKU KUUZA, KUNUNUA MAZAO KWA KUPIMA KWENYE NDOO, MADEBE

    July 12, 2024
  • KAMA UNATAKA MALI UTAIPATA SHAMBANI

    July 11, 2024
  • Tazama zote

Video

WANAFUNZI DARASA LA SABA WAASWA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Zabuni za Manunuzi
  • Zabuni za Ujenzi
  • Huduma

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Tanzania
  • GAIRO ONLINE TV
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Mawasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.

    Sanduku la Posta: 40, GAIRO

    Simu ya Mezani: +255 787730665

    Simu ya Kiganjani: +255 717222572

    Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa