Na. Cosmas Mathias Njingo. GAIRO DC
Wiki chache baada ya Serikali ya awamu ya sita, inayo ongozwa na Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kutangaza orodha ya Watumishi wapya Kumi sa Sita Elfu Mia Sita Sabini na Sita (16,676) wa kada za Afya na Elimu, kati ya 110 waliokuwa wamepangiwa Halmashsuri ya Wilaya ya Gairo wameanza kuripoti ambapo hadi sasa zaidi ya watumishi 90 wamekamilisha taratibu za kiutumishi tayari kuwapangiwa vituoa vyao vya kazi.
Kati ya watumishi wote 110 wa ajira mpya waliopangiwa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Watumishi 105 wa kada zote mbili wamesharipoti na kukamilisha taratibu zote za kiutumishi ikiwepo kukaguliwa vyeti vyao vya elimu ya Sekodari na Taaluma, kujaza mikataba ya ajira, taarifa binafsi za mtumishi, upimaji wa afya pamoja na kuwasilisha akaunti za benki kwa ajili ya kupokelea mishahara yao na kuwasilisha barua za maombi ya posho ya kujikimu mara baada ya kuwasili katika vituo vyao vya kazi.
Idadi hii ya watumishi waliopangiwa kuripoti Gairo angalau kwa kiasi kidogo itasaidia kupunguza uhaba wa watumishi kwa baadhi ya vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na kupata watumishi kwa zahanati mpya sambamba na kuongeza walimu kwa baadhi ya shule za Sekondari na Msigi zilizokuwa zikikazbiliwa na changamoto ya Uhaba wa Watumishi.
Kada ya Elimu imepangiwa jumla ya Walimu 58, kati yao 21 ni Walimu wa shule za Sekondari wakati Elimu Msingi imapata jumla ya walimu 37, ambapo kwa idadi hiyo changamoto ya uhaba wa Walimu imepungua kwa kiasi kidogo angalau itasaidia badhi ya shule zilizokuwa na walimu wachache zaidi hapo awali kupata walimu wa nyongeza kwa ili kuongeza kasi ya kufundisha na kujifunza.
(Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi Bi Emma Kibona)
Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi Bi. Emma Kibona amesema kati ya Walimu 37 walioajiriwa kufundisha shule za Msingi Wilayani Gairo Walimu 32 wameripoti kazini huku akitaja walimu 5 bado hawajaripoti na kwamba anatarajia Walimu hao waliosalia watawasili wakati wowote kuanzia sasa, na kuongeza kuwa kupata walimu hao 37 kutaongeza nguvu kazi kwa baadhi ya shule, kuinua kiwango cha taaluma na ufaulu.
"Kwa upande wa Idara ya Elimu Msingi tunaishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Mama yetu kipenzi Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan angalau mwaka huu imetuona na kutuletea Walimu 37, kati yao Wanaume ni 19 na Wanwake 18, lakini hadi sasa tayari Walimu 32 wamesha ripoti na wengine wapo kwenye vituo vyao vya kazi kuendelea na majuku ya kule, wamebaki Walimu 5 tu ambao tunaamini kwa muda huu mchache uliosalia watawalisi tayari kukamislisha taratibu za kiofisi na kwenda kuripoti kwenye Shule zao walizopangiwa", alifafanua Bi. Kibona.
Aidha kibona alieleza kuwa Walimu hao 37 kwa uchache wao angalau wataongeza nguvu kazi kwenye baadhi ya maeneo hasa shule zilizokuwa na uhaba mkubwa wa Walimu na kwamba kwa kiasi fulani itaongeza morali ya kufundisha na ufundishaji kwa shule hizo na kuinua kiwango cha ufaulu, ambapo pia aliongeza kuwa bado changamoto ya upungufu wa Walimu kwa shule za Msingi ni kubwa ilinganishwa na idadi ya Walimu ambao wameajiriwa na kupangiwa katika Halmashauri hiyo.
"Pamoja na shukrani zetu kwa Rais Mhe. Mama Samia Suluhu Hasssan kwa kutuletea Walimu, bado tunamuomba asitusahau tena kwa awamu ijayo wakati wa kupanga Watumishi wa Ajira mpya kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa kwani Gairo tuna upungufu wa Walimu 379 kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya shule zetu. Najua siyo rahisi kuwaleta wote kwa wakati mmoja kutokana na ufinyu wa bajeti, angalau tuletewe wa kutosha hasa katika shule ambazo zinaupungufu zaidi. Hata Walimu waliopo kwa sasa hawatoshi kufikia wastani ambapo shule moja inatakiwa kuwa na walimu angalau 8, likini shule nyingi zina Walimu chini ya 6 pungufu zaidi ya uhalisia". Alifafanua
(Bi Nivoneia Levery ni Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari)
Walimu wa Elimu Sekondari walioripoti hadi kufikia taarifa hii kuandaliwa walikuwa 21 sawa na 100% ya walumu wote waliopangiwa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo hivyo kufanya upungufu wa Walimu shule za sekondari kufikia 43 kutoka Walimu 64 hapo awali kabla ya ajira mpya.
Bi Nivoneia Levery ni Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Gairo anasema amepokea Walimu hao wa Ajira mpya kwa furaha kubwa na kwamba ujio wao utakuwa na tija katika kuleta mapinduzi ya kitaaluma kwa kuongeza ari ya kufundisha na kujifunzia, hali ambayo ametaja itapandisha kiwango cha taaluma na kuongeza ufaulu hasa kwa masomo ya sayansi ambayo yalikuwa yakikabiliwa na uhaba wa walimu wa masomo hayo.
(Bi Nivoneia Levery ni Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari)
"Kwa kweli nimefurahi sana kupata walimu 21 angalau uhaba wa Walimu unazidi kupungua hadi Walimu 43 kuto upungufu wa 64 uliokuwepo hapo awali kabla ya Serikali kutuletea Walimu wa Ajira Mpya ambao wote 21 wamesha ripoti Halmashauri kwa ajili ya kukamilisha taratibu zote za msingi na baadaye wakaenda kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi walivyo pangiwa na Wizara", Alisema Bi. Levery
Sambamba na kupokea walimu hao 21 wa Ajira mpya Mkuu huyo wa Idara ya Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Gairo alibainisha kuwa Halmashauri hiyo ina jumla ya shule za Sekondari 15 ambazo zote zimesajiliwa na zinaendelea kutoa huduma kwa jamii na kuongeza kuwa shule 1 mpya ipo kwenye katua za mwisho za kumalizia ujenzi wake hivyo kufikia idadi ya Shule 16 ambapo shule hiyo inatarajiwa kuanza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka wa masomo 2023.
Alisema "Halmashauri yetu ina jumla ya kata kumi na nane (18), shule za Sekondari zipo kumi na tani (15), hivyo utaona kata tatu (3) zinakosa shule, lakini tunatarajia kufungua shule mpya moja (1) ya Sekondari katika kata ya Leshata Januari 2023, shule hii inajengwa kupitia Mradi wa SEQUIP na itaanza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza wa kata ya Leshata na vijiji vya kata jirani ili kupunguza adha wa Wanafunzi kulazimika kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kufuata huduma za elimu ya sekondari".
(Bi Nivoneia Levery ni Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari)
Mkuu huyo wa Idara ya Elimu Sekondari akaiomba Serikali kuongeza Walimu katika zoezi lijalo la kuajiri kwa kuwa bado kuna uhaba wa walimu 43, huku akichanganua kuwa Walimu thelathini na mbili (32) wa masomo ya Sayansi wanahitajika, wawili (2) wa masomo ya Biashara, Hisabati kumi na nne (14) na kiingereza Walimu kumi na nne (14).
(Bi Nivoneia Levery ni Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari)
"Bado uhitaji wa walimu ni mkubwa kwani shule zinaongezeka na wanafunzi pia wanaongezeka, hivyo ninaomba Serikali yetu sikivu kupitia Wizara ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kuingalia Gairo kwa jicho la tatu ikiwezekana, na kama itampendeza Mhe. Bashungwa kuongeza idadi ya Walimu angalau wapatikane wengi kwa masomo ya Sayansi, Hisabati na Kiingereza. Pia tunauhitaji wa Walimu wawili (2) wa masomo ya Baiashara". Aliomba Bi. Levery
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa