Na Cosmas Mathias Njingo, GAIRO DC
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kasimu Majaliwa (MB) ameupongeza Mkoa wa Morogoro kwa kutekeleza kwa vitendo kampeni ya upandaji miti ili kuhakikisha Mkoa unarejesha Uoto wa asili kupitia kampeni inayolenga kupanda,kutunza, kuhifadhi na kulinda mazingira ya Misitu ndani ya Mkoa huo ambapo pongezi hizo zimeenda sambamba na tuzo ya Utambuzi katika Kampeni ya Utunzaji wa Mazingira.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akimkabidhi Tuzo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela (kushoto) ishara ya kutambua mchango wa Mkoa huo kushiriki kwenye kampeni za upandaji miti. Katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jaffo. TUZO hiyo imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais leo Juni 5 2022
Tuzo ya Utambuzi wa Mchango wa Mkoa katika upandaji miti na uhifadhi wa mazingira imetolewaJuni 5.2022 na Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassima Majaliwa katika hafla fupi ya kukabidhi tuzo hiyo iliyohudhuliwa na viongozi mbalinbali wa Mkoa akiwepo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Martine Shigella, Wakuu wa Wilaya na badhi ya wajumbe wa Kuu Mkoa.
Akikabidhi tuzo hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Martine Shigella, Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa aliwapongeza Wananchi wote wa Mkoa kwa kuitikia wito wa Serikali wa kuhakikisha kila mmoja anashiriki kikamilifu katika swala la upandaji, utunzaji miti na uhifadhi wa mazingira na kuongeza kuwa Mkoa wa Morogoro umefanya vizuri katika kutekeleza kampeni hiyo ya upandaji miti kwa asilimia kubwa ikilinganishwa na mikoa mingine.
"Napenda kwapongeza wana Morogoro kwa kuitikia wito wa kampeni ya kupanda miti na kuhifadhi mazingira, kampeni hii inalenga kurejesha ustawi wa uoto wa asili ambao tuliuharibu sisi wenyewe kwa shuguli mbalimbali za kibinadamu. Wito wangu kwenu miti mliyoipanda mjitahidi kuitunza ili ikue vizuri badala ya kuiacha ife kwa kukosa matunzo", alisema Mhe. Majaliwa.
Mapema hivi karibuni kabla ya kuanza utekelezaji wa Kampeni ya upandaji miti, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Shigella alitaja mikakati ya kurejesha uoto wa asili ndani ya Mkoa wake waakati wa ufunguzi wa Kongamano la Mazingira lililofanyika ukumbi wa Magadu Mess Manispaa ya Morogoro, tukio hilo liliambatana na shughuli ya upandaji wa Miti katika Shule ya msingi ya Magadu kama sehemu ya kutekeleza mkakati huo.
Mikakati iliyopangwa na Mkuu wa Mkoa huo akishirikiana na Viongozi wa chini yake wakiwemo Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri, viongozi wengine wa chama na Serikali, ni kuhakikisha taasisi za Serikali zikiwemo shule za Msingi na Sekondari pamoja na wadau wengine kuwa wanapewa miche ya miti kwa ajili ya kupanda na kurejesha uoto wa asili ndani ya Mkoa huo.
"Mkaka mmoja wapo ni kuhakikisha kila kiongozi ngazi ya Wananchi Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Umma na Binafsi ni lazima washiriki kwenye kampeni hii kwa kuhakikisha miti inapandwa kwa wingi na ya kutosha kwenye maneo na tasisi zao, zikiwepo shule zote za Msingi na sekondari", alieza Mkuu wa Mkoa Mhe. Shigella.
Mikakati hiyo ambayo imekuwepo tangu mwaka mmoja uliopita ndio haswa umeaanza kuonesha matokea chanya ya uoto wa asili kuanza kurejea taratibu katika baadhi ya maeneo lakini pia na Serikali kuanza kutambua mchango wake katika kampeni ya Upandaji miti na kutoa TUZO kwa MKoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Shigela akipanda mti
Mhe. Shigela akizungumza na wadau mbalimbali wa Mazingira , kulia kwake ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Mhe. Pascal Kihanga
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Martine Shigela (wa pili kushoto) akiwa katika Maandamano na wadau wengine wa mazingira wakielekea eneo la kupanda miti siku ya Kongamano la wadau wa Mazingira lililofanyika mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame akionyesha TUZO ya Utambuzi Mkoa wa Morogoro katika kampeni ya Upandaji Miti, iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais. Wilaya ya Gairo Kupitia Kampeni ya URITHI WA KIJANI ni mdau mkubwa katika kufanikisha upatikani wa TUZO hiyo muhimu kwa Mkoa wa Morogoro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa