Na. Cosmas Mathias Njingo
Sept. 13.2022.
Serikali Wilayani Gairo Mkoani Morogoro, imesema imejipanga kuunda timu maalum ya kuhakikisha inaweka mikakati nadhubuti ya kupambana dhidi ya vitendo vya ukatilia wa kijinsia na kingono vivyokithiri miongoni mwa jamii, ili kujenga Taifa imara lenye maadili na nidhamu bora.
Kauli hiyo imetolea Septemba 13.2022, na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame wakati wa kikao cha Kamati ya Sensa Wilaya, cha majumuisho na tathimini ya utekeleaji wa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi lililofanyika kuanzia Agosti 23.2022. Ambapo Wilaya ya Gairo imefanya vizuri kwa mkoa wa Morogoro baada ya kupita lengo la kuhesabu kaya kwa kufikia asilimia 126.9
“Tumejipanga kuunda timu maalum ambayo kazi yake kubwa itakuwa ni kufanya ufuatiliaji wa karibu wa taarifa zote za uwepo wa vitendo vinavyoashiria ukatili wa kijinsia na kingono, hii ni sambamba na kuwabaini wale wote wanaoripotiwa kuhusika kutekeleza vitendo hivyo katika jamii”. Alisema Mhe. Makame.
Mhe. Makame amesema ofisi yake itashirkiana kwa ukaribu na Timu hiyo ambayo aliwataja Wajumbe wake kuwa ni Dawati la Jinsia kutoka Jeshi la Polisi Wilayani humo, Kitengo cha Ustawi wa Jamii cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Idara ya Maendeleo ya Jamii pamoja na Afisa kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
“Kesi za Ukatili wa Kisinsia na Kingono zimekuwa zikiripotiwa kwa wingi, lakini kumekuwepo na udhaifu mkubwa katika kusimamia utatuzi wa changamoto hii, hivyo kupitia timu hii tutaenda kukomesha kabisa matukio ya namna hii, na lengo letu kama Wilaya ni kuhakikisha hakuna tena kesi za ujkatili wa kijinsia”. Alifafanua Mkuu huyo Wa Wilaya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa