Na. Cosmas Mathias Njingo, DAR ES SALAAM.
Juni 21.2024
Serikali imesema itaviwezesha vitengo vya Mawasiliano Serikalini kwa kutoa vitendea kazi ili kupunguza changamoto ya ukosefu wa vifaa kutokana na ufinyu wa Bajeti za Halmashauri za Majiji, Maniispaa, Miji na Wilaya.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Mawasilino na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nauye (MB), akifunga kikao kazi cha 19 cha Maafisa Habari wa Serikali katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City Jijini Dar Es salaam Juni 22. 2024.
“Serikali imesikia kilio cha Maafisa Habari, na inatambua changamoto ya ukosefu wa Vitendea kazi hasa Kamera. Sasa; Wizara ninayoiongoza Mimi, itatoa vifaa vya kisasa kwa Maafisa Habari wa Halmashauri kote nchini, ili kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi”. Alisema Mhe. Nape.
Na kuonge kwa kusema “Tunataka kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kila Afisa habari awe amepata vitendea kazi. Lengo la Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia, ni kuhakikisha vitengo vya mawasiliano Serikalini vinakuwa na nguvu kubwa na uwezo wa kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu katika kutangaza shughuli za Serikali hasa Miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Awali akimkaribisha Waziri Nape kufunga kikao kazi hicho, Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Habari Maelezo Bwn. Thobias Makoba alisema kikao kazi hicho kimekuwa na mafanikio makubwa kwani kimewapa fursa maafisa Habari wa Serikali kujifunza mbinu mpya na kuwaongezea ujuzi utakao saidia kuboresha utoaji wa taarifa kwa umma.
“Mhe Waziri nichukue fursa hii kukujulisha kwamba, kikao kazi hiki kimekuwa na manufaa makubwa sana kwa Maafisa habari wa Serikali kwani mada zilizowasilishwa zimewasaidiakujifunza mambo mengi ambayo tunaamini yataleta mabadiliko hasa mbinu walizozipata za namna ya utoaji wa taarifa stahuki kwa Wananchi”.
Pamoja nayao Makoba alisema kupitia kikao kazi hichio, Maafisa Habari hao waliweze kujadili changamoto mbalimbali zinazowakwamisha katika utekelezaji wa shughuli zao za kila siku, pamoja na kuweka mikakati ya pamoja ya kutafutia ufumbuzi changamoto hizo.
Kikao kazi hicho cha siku 2, kilianza Juni 21 khadi Juni 22. 2024, kilitanguliwa na Kongamano la Wadau wa Sekta ya Habari lililofunguliwa na Mhe. Dakta Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Juni 19.2024.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa