Na. Cosmas Mathias Njingo. GAIRO
Juni 1. 2024.
Baraza la Wahe. Madiwani wa Halmashuri ya Wilaya ya Gairo wameshaishauri Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kuweka utaratibu wa kuwapongeza wakusanya mapato na Kata zinazofanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato, hususani zilizovuka lengo la makusanyo ili kuongeza bidii ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri.
Wametoa ushauri huowakichangia taarahfa za mapato kwa kila Kata zilizowasilishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la kupokea na kujadili taarifa za maendelo ya kata kipindi cha Robo ya Tatu cha Januari Machi 2023/2024 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri mei 23.2024.
Diwani wa Kata ya Italagwe Mhe. Yosia akichangia hoja ya Mapato, ambapo amesisitiza kuwa ucheleweshaji kurudisha kwa asilimia za Vijiji na Kata ili kuwawezesha Halmashauri kupata Mapato mengi ya kutosha kutosha kuendeleza miradi mingine ya maendeleo inayoteklezwa kwa fedha za mapato ya Ndani.
Mhe Masatu Butindi Diwani wa Kata ya Kibedya, akichangia hoja hiyo, amepongeza Kata za Gairo na Rubeho kwa kuvuka lengo la makusanyo na kushauri kuwa kuwepo na utaratibu wa kutoa zawadi au kuziandikia barua Kata zilizofanya vizuri kwenye zoezi hilo la ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali.
Butindi ameikumbusha Halmashauri kuhakikisha fedha za madeni mbalimbali ikiwepo madeni ya Stahiki za Wahe. Madiwani, madeni ya Watumishi, Wazabuni na Watoa huduma mbalimbali wanalipwa kabla ya mfumo kufungwa ifikapo Juni.30.2023.
Kwa upande wake Mhe. Frank Mbaigwa Diwani Kata ya Ukwamani aliunga mkono hoja ya kuzipongeza kata zinazofanya vizuri katika zoezi la kukusanya mapato na kuongeza kuwa ni vyema pongezi hizo ziambatane fedha kidogo ilikuwatia moyo wakusanya mapato badala ya kuwaandikia barua peke yake za kuwapongezas
"Kata zinazofanya vizuri kwenye zoezi la ukusanyaji wa mapato zisiishie kuandikiwa barua za pongezi peke yake,barua hizo ziambatane na bahasha zenye chochote kitu ndani, hii itasaidia sana kuwatia moyo Watendaji wetu na kuongeza morali ya utekelezaji wa jukumu la kukusanya mapato. Na sisi Waheshimiwa Madiwani tufanye kama ilivyofanyika kwenye wiki la Elimu, Walimu waliofaulisha vizuri masomo yao walipongezwa kwa bahasha". Mhe. Frank Mbaigwa Diwani Kata ya Ukwamani.
Mhe. Mbaigwa alitoa ushauri huo kufuatia taarifa za Kata za Gairo na Rubeho kuvuka lengo la makusanyo kwa kipindi cha robo ya tatu zaidi ya 100% huku utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa Fedha 2023/2024 ukielekea ukingoni, ambapo kuanzia Julai Mosi 2024 Halmashauri itaanza kutekeleza bajeti ya mwaka mpya wafedha 2024/2025.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa