Na Cosmas Mathias Njingo, GAIRO
Aprili 24. 2024
Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 zimepokea na kuridhia taarifa ya Ujenzi wa Mradi wa Zahanati ya Kijiji cha Ng'holingo kilichopo Kata ya Madege na kisha kuweka jiwe la Msingi Aprili 22.2024. Mradi umelenga kusogeza huduma za Afya kwa Wananchi wa Kijiji cha hicho, ikiwa ni pamoja na huduma za Mama na Mtoto ili kupunguza gharama za kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za Afya.
Mradi umegharimu jumla ya Shilingi 83,745,093.7 ambazo zinatokana na michango ya fedha, vifaa vya ujenzi na nguvu kazi kutoka kwa wananchi vyenye thamani ya Shilingi 27,945,093.79, Mhe. Diwani kata ya Madege aliyechangia Mawe tripu 7 na mchanga tripu 5 zenye thamani ya Shilingi 360,000.00, Mfuko wa Jimbo Bati 206 na Misumari ya bati kg 25 yenye thamani ya Shilingi 5,440,000.00, na Fedha kutoka Serikali kuu Sh4.1.5.1 na kufanya fedha yote kufikia kaisi cha Shilingi 50,000,000.00.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa