Waumini wa Kanisa la Anglikana Wilayani Gairo Dayosisi ya Morogoro mwameadhimisha kumbukumba ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume kwa kuzindua kampeni ya kupanda miti na kuhamasisha Wananchi wote wilayani humo kupanda miti kwa wingi kuzunguka maeneo yao ili kuweka mazingira yawe nadhifu kuepuka hali ya jangwa.
Kampeni hiyo ya upandaji miti kwa waumini wa Kanisa la Anglikana imezinduliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe, April 7.2017 kwa kupanda kuzunguka eneo la kanisa hio.
Askofu wa Anglikan Dayosis ya Morogoro Godfrey Hadadi Sehaba alisema swala la uhifadhi wa mazingira ni jambo mtambuka na kwamba kila mwananchi analazimika kuhakikisha anapanda miti ya kutosha sambamba na kuhifadhi mazingira.
“Sote kwa pamoja tunawajibika kupanda miti na kiutunza ili itusaidie kuhifadhi uoto wa asili ambao ni chanzo kizuri cha mvua”, alibainisha Askofu Sehaba,.
Aidha aliwataka wananchi na waumini wa kanisa hilo kuondokana na imani potofu za kishirikina kuwa kukosekana kwa mvua chanzo chake ni waganga wa kienyeji wakituhumiwa kuhusika kuzuia mvua zisinyeshe.
“Wachawi wa mvua ni sisi wananchi wenyewe, kutokana na tabia zetu za uharibifu wamzingira nakukata miti hovyo, hivyo ni rai yangu wa wananchi wote kuacha kusingizia waganga wa kienyeji kuhusika na ukosefu wa mvua”, alifafanua.
Akihutumia Wananchi waliohudhuria uzinduzi huo wa upandanji miti, Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe alisema ni vyema kila mkuu wa kaya ahahakikishe angalau anapanda miti isiyopungua 3 kuzunguka eneo lake la makazi, na kuongeza kuwa mfmo huo utarejesha Gairo katika hali nadhifu.
“Napenda kuona Gairo mpya ikiwa na mazingira safi na nadhifu, nitafarijika zaidi nkiona kila kaya inamiti isiyopungua mitatu, na ni vyema ikapandwa kwenye mipaka ya viwanja ili kuondokana na migogora ya aridhi”, alieleza Mkuu wa Wilaya.
Aidha Mkuu huyo wa wilaya alisisitiza swala la kulinda na kuenzi tunu ya amani na utulivu vilivyoachwa na viongozi waasisi wa Taifa la Tanzania kwa kuhakikisha kila mmoja anatii sharia bila kusudi sambamba na kupuka vitendo vya kihalia ikiwepo wizi, ulevi na matumizi ya dawa za kulevya.
“Mimi na kamatia yangu ya ulinzi na usalama tunaendelea kuhakikisha Gairo ipo salama, hivyo basi nanyi nawaomba muwe mabalozi wa ulinzi na usalama kwa kutii sharia bila shuruti na kutojihusisha na vittendo vya kihalifu”, alisisitiza Mhe. Mchembe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 715240010
Simu ya Kiganjani: +255 715240010
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa