SERIKALI imesema itaweka utaratibu mzuri wa kufanya utafifi wa kina ili kutumia vyanzo vya maji vilivyoko milima ya Masenge sambamba na kujenga miundombinu mipya ya mtandao wa maji safi Wilayani Gairo ili kuondoa tatizo la upatikanaji wamaji safi na salama Wilayani humo.
Huu utakuwa mwarobaini wa tatizo la ukosefu wa huduma za maji ya uhakika kwa wakaazi wa Gairo lililodumu kwa muda mrefu ingawa miradi mingi ambayo imekuwa ikitekelezwa kwa kutumia fedha nyingi za Umma na Wahisani haikuleta matoke chanya.
Hivi karibuni Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alizungumza na wakazi wa Wilaya ya Gairo wakati akipita kutokea Dar es salaam kuelekea Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine, Mhe. Mama Samia aliwambia wakazi hao kuwa Serikali inatambua vyema shida ya maji iliyopo Gairo.
"Tatizo la maji kwa Wanagairo nalifahamu, na hata ule mradi mkubwa uliofadhiliwa na Benki ya Dunia naufahamu vuzuri sana, sasa ipo mikakati kadhaa ya kuhakikisha tunapata maji ya uhakika kwa kutumia vyanzo vilivyopo". Alibainisha Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Samia alisema Benki ya Dunia ilitoa kiasi cha Shilingi bilioni 6 kwa ajili ya kutekeleza mradi mkubwa wa maji Wilayani Gairo ili kukabiliana na shida ya maji inayowakabili wananchi ambapo jumla ya Shilingi bilioni 2 zimekwishatumika hadi sasa bila mfanikio yoyote hivyo kiasi cha fedha kilichobaki kitatumika kutafuta ufumbuzi wa swala hilo.
alisema "Tumejipanga vyema kushughulikia tatizo lenu wanagairo, hivyo naomba mniamini, jambo hili nimelibeba na nitalishughulikia, zipo shilingi bilioni mbili bado hazijatumika, ambazo tunalenga zitatumika katika kufanya tafiti za namna ya kutumia maji yanayopatikana masenge, pamoja na kuweka miundombinu safi ya mtandao wa maji, hili linawezekana".
Nao baadhi ya Wanachi wakizungumza mara baada ya Mhe. Samia kuondoka, walisema endapo Serikali itatoa kipaumbele kwa Wilaya ya Gairo katika kutatua tatizo la ukosefu wa maji safi na salama, itakuwa imeokoa wananchi wengi kwani kwa sasa maji yanayotumika hayatoshelezi mahitaji kwa siku ikilinganishwa na idasdi ya watu waliopo Wilayani humo.
Demolished smashed
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 715240010
Simu ya Kiganjani: +255 715240010
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa